Said, Rahma Mohammed
(2019)
Kuchunguza Uhalisiajabu katika Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza uhalisiajabu katika Riwaya ya Mzimu wa Watu wa
Kale. Utafiti huu ulihusisha malengo mahsusi mawili ambayo ni kubainisha
vipengele vya uhalisiajabu katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale na lengo la pili
ni kubainisha dhamira zinazojidhihirisha kutokana na matumizi ya vipengele vya
Uhalisiajabu katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale. Katika kuyabainisha na
kuyachambua malengo haya, mtafiti ametumia mbinu ya usomaji makini pamoja na
upitiaji wa nyaraka maktabani. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu
ya madhumuni maalumu. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia
mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu uliongozwa na Nadhariaya Uhalisiajabu kwa lengo
mahsusi la kwanza na suali la kwanza. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji imetumika
kwa lengo mahsusi la pili na suali la pili katika muktadha wa Uchambuzi wa Matini
za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwariwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale imetumia
vipengele vya uhalisiajabu ambavyo ni wahusika wa kihalisiajabu, mandhari ya
uhalisiajabu, uzungumzi nafsi, matukio ya kihalisiajabu, usimulizi wa kihalisiajabu
na umahuluti wa kitanzu, kitamaduni na mwingilianomatini. Adha, utafiti
umegundua kuwa vipengele hivyo vya uhalisiajabu katika riwaya teule vimeibua
dhamira za imani za jadi, uongozi mbaya, ukoloni, utabaka, mauaji, umuhimu wa
kutunza kumbukumbu, upelelezi, uganga wa kienyeji, unyonyaji na ukandamizaji na
nafasi ya mwanamke. Kwa matokeo haya utafiti huu umebaini kwamba riwaya ya
Mzimu wa Watu wa Kale imesawiriwa kwa mbinu ya uhalisiajabu kwa kiasi kikubwa
kama mtindo wa msanii kuibua dhamira alizozikusudia kwa jamii aliyoiandikia.
Actions (login required)
|
View Item |