Haji, Amina Makame
(2019)
Maana za kimuktadha zilizojitokeza katika semi zilizoandikwa katika majina ya kanga.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza Maana za Kimuktadha zilizojitokeza
katika Semi
zilizoandikwa katika Majina ya Kanga. Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu ya
msingi. Malengo hayo ni Kubainisha semi mbali mbali zilizoandikwa katika kanga
kutegemeana na maudhui zake. Kubainisha maana za semi teule zilizoandikwa
kwenye kanga kwa kuangalia maana ya msamiati na muktadha na Kuchambua
maana za muktadha ya semi teule zilizoandikwa
kwenye kanga. Mbinu za kukusanyia data za utafiti huu zilkuwa ni mahojiano na
uchunguzi makini. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa mkabala wa kimaelezo huku
ukiongozwa na nadharia tatu. Nadharia hizo ni Maana Kimatumizi, Maana
Kimuktadha na nadharia ya Simiotiki. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa kuna
semi mbalimbali zilizotofautiana kimaudhui ambazo zimeandikwa katika kanga.
Semi hizo zimejikita katika maudhui ya mila na utamaduni wa jamii, dini na imani,
maarifa mengineyo, bidii katika kazi na subirá na uvumilivu. Kwenye lengo la pili,
matokeo yalionesha kuwa maana za semi zinajikita kimsamiati na kimuktdha. Maana
za kimsamiati huibuka kutokana na vijenzi mahususi vilivyojenga usemi wenyewe.
Maana za kimuktadha zinatokana na tafsiri mahususi inayotokana na mtazamo na
muktadha wa kimatumizi kama inavyofahamika na jamii husika. Na katika lengo la
tatu amegundua kuwa semi zilizo katika maudhui mbalimbali huandikwa kwenye
kanga ili kufikisha ujumbe maalum kwenye jamii ambapo kanga huvaliwa. Semi
hizo kukanya, hukosoa na hata kuelekeza juu ya utendaji bora wa mambo katika
jamii husika. Kwa mfano maswali ya wivu uliokomaa ulizungumziwa, umuhimu wa
kubaki kwenye ndoa, umuhimu wa kuheshimiana, umuhimu wa bidii ya kazi, subirá
na uvumilivu na maadili kadha ya kijamii yalihusishwa kwenye lengo hili la tatu.
Actions (login required)
|
View Item |