Mbarouk,, Issa Khamis
(2017)
Kuchunguza Tamathali za Semi katika Kuibua Dhamira katika Riwaya ya Mbali na Nyumbani.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu uchunguzi wa tamathali za semi katika kuibua dhamira katika riwaya ya Shafi Adam Shafi. Mbali na Nyumbani. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya tamathali za semi katika riwaya ya Mbali na Nyumbani (2013) ya Shafi Adam Shafi, ili kuona jinsi gani tamathali zimetumika kisanii katika kuibua dhamira katika kazi hii. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalum, wakati ambapo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mapitio ya maandishi. Data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Uchunguzi, uchambuzi na mjadala wa matokeo ya utafiti huu yaliongozwa na nadharia ya Simiotiki.Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, Shafi Adam Shafi ametumia tamathali za semi kama mbinu ya kimtindo katika kuibua dhamira za kazi yake. Hii ni kusema kwamba Shafi Adam Shafi anaendelea kuitumia mbinu ya tamathali za usemi kama kibainishi chake cha mtindo katika kazi zake za riwaya. Riwaya ya Mbali na Nyumbani imeathiriwa zaidi na matumizi ya tashibiha ikifuatiwa na tashihisi na tamathali nyengine zimetumika katika kuongeza nguvu ya ufahamu wa riwaya hiyo.
Actions (login required)
|
View Item |