Ali, Daud Moh’d
(2017)
Kuchunguza Maudhui ya Nyimbo za Kampeni za Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2000-2010.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umechunguza maudhui ya nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu, Zanzibar (2000-2010). Mtafiti aliongozwa na madhumuni mahsusi matatu, la kwanza, kuchunguza na kuainisha nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu, Zanzibar 2000-2010, la pili, Kutathmini mchango wa nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu Zanzibar, katika kustawisha jamii ya Wazanzibari, na la tatu, Kutafuta mbinu za kufanya nyimbo hizo ziwe zinaleta umoja badala ya utengano katika jamii ya Wazanzibari. Katika kufanikisha madhumuni hayo, mtafiti alifuata njia zilizostahiki kwenda kwenye vikundi vya ngoma na kukutana na malenga ili kupata data alizozihitaji kwa watafitiwa. Watafitiwa hao waligawanyika katika makundi ya vijana, watu wazima wenye maarifa na kumbukumbu za mambo ya kihistoria, walimu, wasanii, wataalamu wa lugha ya Kiswahili na utamaduni, na waandishi wa habari. Mtafiti aliongozwa na nadharia ya mtu na Utamaduni, nadharia ya Fasihi ina kwao, nadharia ya Tabia na nadharia ya Uhalisia katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti. Aidha, utafiti umetaja kipengele cha lugha, wahusika na mandhari ili kuibulia maudhui yaliyokusudiwa. Utafiti umeonesha dhamira ya kuhamasisha, ajira kwa vijana, na mmomonyoko mkubwa wa maadili ya jamii. Mwisho, utafiti umetoa mapendekezo kwa watafiti wa usoni.
Actions (login required)
|
View Item |