Massuod, Ismahan Abulkasim Essa
(2018)
Kuchunguza Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Alikiona.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona. Katika kufanikisha lengo hili, utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili ambapo lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua usawiri wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona na kuelezea uhalisia wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona kwa jamii ya leo. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji matini na upitiaji wa nyaraka. Data za utafiti zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Ufeministi. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usawiri wa mwanamke unajitokeza katika maeneo ya mwanamke ni uzinzi, mwanamke ni mtu wa hila na ghilba, mwanamke ni mpenda ufahari, mwanamke ni muongo, mwanamke na mmbeya, mwanamke na ujanja, mwanamke ni mtunza kumbukumbu, mwanamke ni stara, mwanamke ni mpenda kupigwa na mwanamke ni mtoa matusi. Usawiri huu wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona umethibitika kuwa na uhalisia katika maisha halisi ya jamii ya Watanzania ambapo mwanamke halisi anafanana na mwanamke ambaye anatajwa katika tamthiliya. Wapo wanawake kadhaa ambao wamekuwa na sifa kama hizo za mwanamke anayetajwa katika Alikiona.
Actions (login required)
|
View Item |