Haja ya lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya Sekondari.Mifano Kutoka Wilaya ya Ilemela-Mwanza

Lunyana, Nicholaus Mvugamake (2015) Haja ya lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya Sekondari.Mifano Kutoka Wilaya ya Ilemela-Mwanza. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of NICHOLAUS_-Tasnifu-24-11-2015.pdf]
Preview
PDF
Download (742kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulikusudia kuchunguza haja ya lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya sekondari kwa kutumia mifano kutoka Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza uhusiano baina ya kutotumika kwa Kiswahili katika ufundishaji wa masomo katika shule za sekondari na kushindwa kwa wanafunzi kupata maarifa yaliyokusudiwa. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi ambayo ni; Kubainisha mambo yanayo changia wanafunzi kukosa maarifa ya elimu ya sekondari, kubainisha athari zitokanazo na kutokutumika kwa lugha ya Kiswahili katika kufundishia elimu ya sekondari na kujadili changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi zitokanazo na kutotumika kwa Kiswahili katika ufundishaji wa elimu ya sekondari. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu ulitumia mbinu za maktaba, hojaji na dodoso. Nadharia iliyotumika kukusanya na kuchambua data za utafiti huu ni nadharia ya Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa, walimu na wanafunzi wanapendelea elimu ya sekondari itolewe kwa lugha ya Kiswahili badala ya kutumia lugha ya kigeni. Utafiti umedhihirisha kuwa, utolewaji wa elimu ya sekondari kwa lugha ya kigeni hauna mafanikio makubwa hata kama kauli mbiu ya sasa ya serikali ni matokeo makubwa sasa. Ni vigumu kupata matokeo makubwa ikiwa wanafunzi hawaelewa wanachofundishwa.Ili kupata matokeo makubwa na yenye ufanisi ni lazima serikali na wadau wote wa elimu waamue kukifanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia elimu ya sekondari.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:08
Last Modified: 13 Jul 2016 10:08
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1439

Actions (login required)

View Item View Item