Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Msondo wa Pembe

Mohd, Asha Rashid (2015) Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Msondo wa Pembe. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_ASHA_FINAL_KISWAHILI_ASHA.pdf]
Preview
PDF
Download (560kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza dhima za nyimbo za ngoma ya msondo. Utafiti ulifanyika katika shehia ya Kengeja, Mwambe na Mkungu- Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini- Pemba. Lengo kuu la utafiti huu ni kukusanya, kuchunguza na kuzianisha dhima za nyimbo za ngoma ya msondo [wa kike]. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya Uamilifu, nadharia ya Simiotiki (Uashiriji), na nadharia ya Sosholojia (Ujamii). Data zilikusanywa kutoka uwandani kwa kutumia mbinu ya usaili na mbinu ya kushirki. Aidha njia ya maktabani ilitumika kwa kusomwa tasnifu tafauti, vitabu na majarida. Matokeo ya utafiti ni dhima zilizopatikana ni dhima ya kuelimisha kwa kuonya, kufunza, na kuhimiza maadili mazuri katika maisha ya ndoa. Aidha, dhima ya kuburudisha maharusi imejitokeza katika nyimbo za ngoma ya msondo. Mafunzo ya nyimbo hizi ambayo yamejitokeza ni ustahamilivu wa shida na matatizo katika ndoa, kumuenzi na kumdhibiti mume au mke, kuwapenda na kuwathamini wakwe, kutunza usafi na kujipamba mke mbele ya mume wake, kuwacha tabia mbaya, kumuheshimu na kumtii mume. Kwa upande wa vipengele vya fani vilivyosaidia kufikisha mafunzo kwa walengwa ni lugha ya ishara, taswira, tashhisi, tauria, tashbiha, kejeli, na kadhalika kama vinavyojitokeza katika uchambuzi wa vipengele hivyo katika sura ya nne.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:36
Last Modified: 13 Jul 2016 10:36
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1275

Actions (login required)

View Item View Item