Kuchunguza Motifu katika Tamthiliya Teule za Emmanuel Mbogo

Mwakanjuki, Ndimyake (2023) Kuchunguza Motifu katika Tamthiliya Teule za Emmanuel Mbogo. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of NDIMYAKE MWAKANJUKI.doc] Microsoft Word - Submitted Version
Download (868kB)

Abstract

Motifu kama kipengele radidi cha kimuundo kimeonesha kuchunguzwa na watafiti wachache katika uga wa tamthiliya ya Kiswahili zikiwemo tamthiliya za Emmanuel Mbogo. Kwa hiyo, tasnifu hii imechunguza motifu katika Tamthiliya Teule za Emmanuel Mbogo ili kukishughulikia kipengele hiki. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi matatu. Kwanza, kubainisha motifu zinazojitokeza katika tamthiliya teule nne, pili, kuchambua namna motifu zinavyoibua dhamira katika tamthiliya teule; na tatu, kuchambua motifu ya taswira katika tamthiliya teule. Data za msingi zilikusanywa kwa mbinu ya usomaji wa maktabani. Data zilizokusanywa ziliwasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo. Mjadala wa data uliongozwa na nadharia za Usosholojia na Simiotiki. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa katika tamthiliya teule, motifu zimesawiriwa vyema na zimeonesha dhamira na motifu za taswira mbalimbali zinazodhihirisha matendo na mienendo ya mwanadamu katika maisha yake ya kila siku. Motifu ya taswira kama shetani, kuanguka kwa pazia la pate, simba na damu zimeonesha kukithiri kwa mauaji, ukandamizaji, uchawi, udhalimu, udhalilishaji wa kijinsia, kuzimwa kwa matumaini ya watu, uchu wa madaraka na uzalendo. Dhamira hizo zilizobainishwa zimetupatia picha halisi ya jamii inayohusika kihistoria, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Motifu hizi zimetumika kama mhimili mkuu wa kuhimiza masuala mbalimbali kupitia dhamira na kujenga motifu za taswira mbalimbali ili kutoa ujumbe na kukamilisha simulizi katika kazi teule. Tasnifu hii inapendekeza kuwa watafiti na wasanii wengine waweze kukifanyia kazi kipengele cha kimuundo cha motifu katika kazi za tamthiliya za waandishi wengine ili kukifanya kizoeleke katika utunzi na uchambuzi wa kazi za tamthiliya kuliko kukiacha kipengele hiki kutumika katika fasihi simulizi, riwaya na ushairi peke yake.

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Khadija Katele
Date Deposited: 14 Aug 2024 08:28
Last Modified: 14 Aug 2024 08:28
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3955

Actions (login required)

View Item View Item