Hamad, Salma
(2023)
Kuchunguza Migogoro ya Uke Wenza katika Semi Zilizoandikwa katika Vazi la Kanga.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza migogoro ya uke wenza inayojitkeza katika semi zilizoandikwa katika vazi la kanga. Ili kutimiza kusudio Hilo mtafiti alikuwa na malengo mahususi matatu; kubainisha semi zilizotumika katika kanga, kufafanua dhamira za semi za kanga na kuthibitisha uhusiano wa semi katika vazi la kanga na migogoro ya uke wenza. Data za msingi zilikusanywa kwa mbinu za ushuhudiaji, mahojiano na usaili. Mjadala wa data zilizowasilishwa uliongozwa na nadharia ya Usosholojia. Kutokana na uchambuzi wa data, matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwapo kwa semi zinazoonesha dhamira mbalimbali zikiwamo zinazohusu uchumi, itikadi, wivu na ujasiri. Dhamira zilizomo katika semi hizo zinasawiri na zinazoakisi masuala mbalimbali yaliyomo katika jamii ya Watanzania. Pia, umeonesha migogoro mbalimbali inayosababishwa na ndoa za uke wenza. Mwisho, utafiti huu unapendekezo kwa watu mbalimbali kwa kufanya uchambuzi wa kina kuhusu dhamira zinazopatikana katika kanga ili kuweza kurekebisha na kujenga jamii mpya endelevu. Pia, utafiti huu unapendekezo kufanyika tafiti za baadae katika uwanja wa semi za kanga pamoja na semi za magari ya ng’ombe.
Maneno Muhimu: Kanga, uke wenza, migogoro
Actions (login required)
|
View Item |