Kuchunguza Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya ya Mondlane na Samora

Ismail, Fatma Hassan (2019) Kuchunguza Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya ya Mondlane na Samora. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA FATMA HASSAN ISMAIL.pdf] PDF
Download (524kB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu ni Kuchunguza Mtindo na Dhamira katika tamthiliya ya Mondlane na Samora. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi mawili ambayo ni, kubainisha vipengele vya mtindo katika tamthiliya ya Mondlane na Samora, na kubainisha dhamira katika tamthiliya ya Mondlane na Samora Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalumu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani kwa njia ya usomaji makini. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya mkabala wa kimaelezo. Aidha, nadharia ya Umitindo ilitumika kwa lengo mahsusi la kwanza, sambamba na swali la utafiti la kwanza. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ilitumika kwa lengo mahsusi la pili pamoja na swali la utafiti la pili. Nadharia zote hizo zilifanikisha vyema kazi yakukusanya, kuchambua na kuwasilisha data za utafiti. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwatamthiliya ya Mondlane na Samora imetumia vipengele vya mtindo vinavyohusu matumizi ya lugha na vile vinavyohusu sajili mbali mbali kama vile barua, matangazo ya redio, mawasiliano ya simu na lugha ya shuleni na jeshini. Dhamira zilizojitokeza ni ukoloni, harakati za kupigania uhuru, umoja wa Bara la Afrika, umuhimu wa elimu, vita na mauaji, mapenzi na ndoa. Dhamira zote zililenga kusawiri uhalisia wa maisha ya bara la Afrika wakati wa ukoloni na wakati wa harakati za kutafuta uhuru kutoka kwa wakoloni. Mtafiti amegundua kuwa Emmanuel Mbogo amekuwa akichota matukio ya kihistoria katika jamii za Afrika kama msingi wa matumizi ya mitindo yake na dhamira zake katika tamthiliya anazozitunga.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 08:53
Last Modified: 21 Sep 2021 08:53
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2900

Actions (login required)

View Item View Item