Moh`d, Fatma Rashid
(2019)
Kuchunguza Dhamira za Mapenzi na Usaliti katika Riwaya ya Mfadhili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu Kuchunguza Dhamira za Mapenzi na Usaliti katika Riwaya ya
Mfadhili. Lengo kuu ni kuchunguza dhamira za mapenzi na usaliti katika riwaya ya
Mfadhili ya Hussein Tuwa. Utafiti huu umehusisha malengo mahsusi matatu ambayo
ni kubainisha dhamira za mapenzi zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili. Lengo la
pili ni kubainisha dhamira za usaliti zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili na lengo
la tatu ni kubainisha mbinu za kisanaa zilivyoibua dhamira za mapenzi na usaliti
katika riwaya ya Mfadhili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwitiko wa
Msomaji katika lengo la kwanza la kwanza na la pili sambamba na suali la kwanza
na la pili na nadharia ya Simiotiki katika lengo la tatu na suala la tatu. Mbinu
iliyotumika kukusanyia data ilikuwa ni mbinu ya usomaji makini pamoja na upitiaji
wa nyaraka maktabaniambapo mtafiti aliisoma kwa kina riwaya teule huku
akidondoa data ambazo hatimae zilijibu maswali ya utafiti huu. Data za utafiti huu
zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Aidha, utafiti huu uliongozwa
na maswali matatu ya utafiti ambapo swali la kwanza lilikuwa ni; Ni dhamira zipi za
mapenzi zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili? Matokeo ya utafiti huu
yameonesha kuwa riwaya teule ya Mfadhili imeonesha mapenzi ya dhati ambayo ni
kati ya baba na mtoto wake wa kambo, mtu na rafiki yake, mapenzi kati ya mtu na
mchumba wake, mapenzi katika ndoa, mapenzi kati ya mtu na wifi yake, mapenzi
kati ya daktari na jamii na mapenzi ya dhati kati ya mkuu wa kazi na wafanyakazi
wake. Kwa upande mwengine kuna mapenzi ya uongo ambayo yamejitokeza kati ya
mke na mume wake wa ndoa, mapenzi ya uongo kati ya mtu na mchumba wake na
mapenzi ya uongo kati ya marafiki. Swali la pili lililoongoza utafiti huu lilikuwa; Ni
dhamira zipi za usaliti zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili? Data za utafiti
zilionesha kwamba dhamira ya usaliti imejitokeza katika ndoa, usaliti katika mtu na
mchumba wake, usaliti kati ya marafiki na usaliti unaofanywa watumishi wa umma
na usaliti unaofanywa na wafanyakazi wa afya. Swali la tatu lililoongoza utafiti huu
lilikuwa; Ni mbinu zipi za kisanaa zinazoibua dhamira za mapenzi na usaliti katika
riwaya ya Mfadhili? Data za utafiti zilionesha kwamba dhamira ya mapenzi na usaliti
zimeibulia kupitia vipengele vya lugha, wahusika na mandhari.
Actions (login required)
|
View Item |