Kuchunguza Usihiri katika Ngano za Zanzibar

Abdulla, Juma Hamad (2019) Kuchunguza Usihiri katika Ngano za Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA JUMA HAMAD ABDULLA.pdf] PDF
Download (849kB)

Abstract

Utafiti huu ulilenga kuchunguza usihiri katika ngano za Zanzibar. Utafiti ulijikita kuchunguza namna vipengele vya usihiri vinavyojidhihirisha katika ngano za Zanzibar na namna vipengele vya usihiri vilivyotumika kuibua dhamira katika ngano teuele. Mtafiti alichagua mada hii kwasababu matumizi ya usihiri alibaini hayajachunguzwa katika ngano za Zanzibar. Utafiti huu ulifanyika uwandani katika ukusanyaji wa data. Maeneo yaliyotumika kukusanya data ni Sizini, Micheweni, na Wingwi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalum. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisiajabu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ngano za Zanzibar zinatumia usihiri katika vipengele vya ujenzi wa wahusika, ujenzi wa mandhari, motifu za safari, ndoto, vyakula,wahusika, matukio mbali mbali Pia utafiti umegundua kuwa vipengele vya usihiri katika ngano za Zanzibar vimetumika kuibua dhamira za ujasiri, malezi, ushujaa, uongozi mbaya, utu, uchoyo, kiburi, uvivu, ukarimu, ujanja, nafasi ya mwanamke, uhalifu, ukoloni na umaskini.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 08:30
Last Modified: 21 Sep 2021 08:30
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2896

Actions (login required)

View Item View Item