Kuchunguza Dhima ya Nyimbo za Harusi za Jamii ya Wamakunduchi, Zanziba.

Mgunda, Zainab Mbwana (2020) Kuchunguza Dhima ya Nyimbo za Harusi za Jamii ya Wamakunduchi, Zanziba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of FINALLY RESEARCH.docx] PDF - Submitted Version
Download (472kB)

Abstract

Nyimbo za harusi zinatumika katika jamii za Kiafrika tangu karne na karne. Wamakunduchi huzitumia nyimbo hizo kuwafunza wanandoa. Mtafiti amefanya utafiti katika shehia tano za mji wa Makunduchi ambazo ni Kijini, Nganani, Kajengwa, Mzuri na Tasani. Lengo ni kuchunguza dhima za nyimbo za harusi kwa jamii ya Wamakunduchi. Utafiti ulikusanya data Maskanini. Mbinu zilizotumika kukusanyia data hizo ni usaili, hojaji na ushiriki. Nadharia tatu zimetumika katika utafiti huu, ambazo ni nadharia ya Maana, nadharia ya Umuundo na nadharia ya Ndani-nje. Nadharia hizi zimeweza kutoa mwongozo kwa mtafiti kuchambua lugha inayotumika katika nyimbo za harusi za Wamakunduchi, na kuibua dhima za nyimbo hizo kwa jamii hiyo. Data zimekusanywa kutoka kwa vijana, wazee na viongozi wa Dini. Data kuu alizokusanya mtafiti ni nyimbo za harusi zinazozungumzia masuala ya usafi, unyumba, kukuza udugu na kukemea ila kwa wanandoa. Sura ya kwanza imeanza na utangulizi ambao umetoa ufafanuzi kuhusiana na nyimbo, historia fupi ya Zanzibar na mji wa Makunduchi. Sura hii imeeleza usuli wa mada, tatizo la utafiti, lengo, madhumuni, maswali ya utafiti, umuhimu, na mipaka ya utafiti. Sura ya pili, imetoa maelezo ya kazi tangulizi na ufafanuzi wa nadharia na jinsi zilivyomsaidia mtafiti. Sura ya tatu, imefafanua mbinu na njia za utafiti, uteuzi wa vifaa vya utafiti, uteuzi wa watafitiwa, ukusanyaji na uchambuzi wa data. Sura ya nne, imeonesha uchambuzi wa data na matokeo ya utafiti huo. Sura ya tano, imetoa hitimisho la jumla la utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa nyimbo za harusi zina dhima kubwa sana kwa wanandoa katika jamii ya Wamakunduchi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Mugisha Kafuma
Date Deposited: 05 May 2021 08:57
Last Modified: 26 Jan 2023 08:31
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2847

Actions (login required)

View Item View Item