Upimaji Kiwango cha Uelewa wa Mofimu za Uambishaji na Unyambulishaji wa Kiswahili Sanifu kwa Wanafunzi wa Sekondari Tanzania

Bunzali, Ndalahwa (2019) Upimaji Kiwango cha Uelewa wa Mofimu za Uambishaji na Unyambulishaji wa Kiswahili Sanifu kwa Wanafunzi wa Sekondari Tanzania. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA M.A KISWAHILI nomal.pdf] PDF
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulipima kiwango cha uelewa wa mofimu za uambishaji na unyambulishaji wa mofimu za maneno ya Kiswahili sanifu kwa wanafunzi wa sekondari Tanzania. Utafiti ulifanyika Mkoa wa Tabora wilaya za Uyui, Nzega na Manispaa. Mtafiti aliongozwa na malengo makuu mawili: Kubainisha kiwango cha uelewa wa wanafunzi kuhusu mofimu tangulizi, fuatishi na kubainisha sababu zinazosababisha wanafunzi wa sekondari kuwa na kiwango kitakachobainika kwenye lengo na. 1. Ili kufikia lengo kuu mbinu tatu za kukusanya data zimetumika: jaribio, dodoso na usaili. Utafiti uliongozwa na nadharia ya utambuzi. Utafiti ulibaini kuwa wanafunzi wanapokuwa kidato cha pili huonekana kama wameielewa mada ya mofimu lakini ufaulu wao hushuka kadiri wanavyopanda kidato cha tatu hadi cha nne. Kuthibitisha hilo, wanafunzi wa kidato cha tatu na nne walionekana kutofanya vizuri walipokuwa wanajibu maswali ya mofimu ikilinganishwa na wanafunzi wa kidato cha pili. Utafiti umebaini sababu zinazosababisha wanafunzi kuwa na uelewa mdogo wa mofimu kwa wanafunzi wa sekondari kuwa ni pamoja na matumizi ya mbinu ya mhadhara yasiyo shirikishi kwa mwanafunzi ambapo mwalimu huonekana anajua kila kitu, mbinu ya kukaririsha inayolenga ufaulu mzuri wakati wa mitihani bila kumjengea mwanafunzi stadi za maisha kwa kumshirikisha kwa vitendo, na wanafunzi kushindwa kuwianisha maarifa mapya waliyojifunza na maisha yao ya kila siku na vipindi vya Kiswahili kwenye ratiba ni vichache. Hivyo, inapendekezwa kuwa kuna haja ya kuziangalia upya mada zingine zinazofundishwa katika ngazi hii ya elimu kama zinaenda sanjari na wakati wa sasa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 26 Nov 2020 09:28
Last Modified: 26 Nov 2020 09:28
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2530

Actions (login required)

View Item View Item