Athari za Kiisimu za Lahaja ya Kimakunduchi katika Kiswahili Sanifu Kinachotumika Shuleni Makunduchi Zanzibar

Saleh, Saleh Abdelsalam Mohammed (2013) Athari za Kiisimu za Lahaja ya Kimakunduchi katika Kiswahili Sanifu Kinachotumika Shuleni Makunduchi Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ATHARI_ZA_KIISIMU._002.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu uliwalenga wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari za Makunduchi zilizo katika wilaya ya Kusini Unguja katika kuchunguza athari za Kimakunduchi katika Kiswahili Sanifu. Pia, walimu wa somo la Kiswahili walishirikishwa kikamilifu. Kwa upande wa wanafunzi, waliotafitiwa ni watoto wenye umri kati ya miaka 10-14 ambao ni wanafunzi wa msingi; na miaka 15 – 20 wanaosoma sekondari. Mbinu kadhaa zilitumika ikiwemo mbinu ya usaili, mbinu ya kutumia hojaji, mbinu ya maktaba, mbinu ya uchunguzi wa maskanini na mbinu ya majaribio. Kila mbinu ilimsaidia mtafiti kwa namna moja au nyingine wakati wa ukusanyaji wa data; na pia wakati wa uchambuzi. Utafiti huu una sura tano. Sura ya kwanza imefafanua usuli wa mada, tatizo la utafiti, malengo na maswali ya utafiti, umuhimu, upeo wake na pia imebainisha kiunzi cha nadharia kilichotumiwa na utafiti huu. Sura ya pili imeelezea mapitio ya maandiko ambapo mna mjadala wa namna fulani kuhusiana maandiko hayo na namna yalivyomsaidia mtafiti katika kazi yake. Sura ya tatu imezungumzia mbinu alizotumia mwandishi katika ukusanyaji wa data yake. Sura ya nne imewasilisha uchambuzi wa data. Katika uwasilishaji huo, sura imeanza kwa kubainisha sifa za kiisimu za lahaja ya Kimakunduchi kwa ujumla, pia imebainisha matumizi ya Kimakunduchi madarasani pamoja na kuonesha athari za lahaja hiyo kwa Kiswahili Sanifu. Sura ya tano imeonesha matokeo ya utafiti ambapo imebainika kwamba yamekidhi haja ya maswali ya utafiti yaliyotumika kama dira ya ukusanyaji wa data. Mwisho, sura ya sita imemalizia kwa kuonesha muhtasari na mapendekezo ya utafiti.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 22 Jan 2016 06:25
Last Modified: 22 Jan 2016 06:25
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/990

Actions (login required)

View Item View Item