Rashid, Hadija Utukulu
(2013)
Mafunzo ya Nyimbo za jando na unyago kwa Jamii ya Wahiyao wa Masasi, Tarafa ya Lulindi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu mafunzo ya nyimbo za jando na unyago kwa jamii ya wahiyao wa Lulindi Wilaya ya Masasi. Utafiti umechunguza ubora na udhaifu wa mafunzo hayo kwa vijana wa jamii hiyo. Utafiti umelenga kukusanya na kuchanganua data, kuhakiki na kuelezea mafunzo ya nyimbo za jando na unyago kwa jamii ya Wahiyao wa Lulindi wilayani Masasi. Utafiti umeweka msisitizo zaidi juu ya mafunzo ya yapatikanayo kwenye nyimbo za jando na unyago kama tanzu ya fasihi simulizi. Nyimbo za jando na unyago zimekuwa na mjadala mkubwa kwa jamii ya wahiyao. Hii imetokana na mwelekeo hasi wa vijana wa kihiyao. Hali hiyo imechochea kufanyika kwa utafiti huu ili kupata ukweli wa yale yanayosemwa na wasemaje wa tatizo hilo.
Actions (login required)
|
View Item |