Dhima ya Ufutuhi Katika Riwaya za Shaabani Robert

Kabeja, Fortunata Moses (2013) Dhima ya Ufutuhi Katika Riwaya za Shaabani Robert. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_KABEJA.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Tasnifu hii imejaribu kuchangia mawazo na fikra za jinsi ya kutumia fasihi ya lugha katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa kupitiya fani ya ufutuhi. Dhima ya ufutuhi katika Riwaya za Shaaban Robert imeathiri wasomaji, watunzi na wapenzi wa lugha ya Kiswahili kwa kiwango cha juu sana. Sura ya kwanza inatoa utangulizi wa ujumla historia ya marehemu Shaaban Robert, maisha yake, familia yake, kazi na ajira zake, mbari zake kwa ujumla na kazi zake za fasihi alizofanya. Sura ya pili inaelezea mawanda yakinadharia, mkabala wakinadharia ambao umetoa mchango katika kazi hii yaani nadharia tete na nadharia kiongozi. Sura ya tatu ni tahakiki za kazi mbalimbali zilizotangulia ikielezea kazi mbalimbali kuhusu ufutuhi na Dhima ya ufutuhi pamoja na maudhui yake katika Riwaya zilizo lengwa. Sura ya nne inafafanua mbinu za utafiti ambazo zimetumika ikiwa ni pamoja na umakinifu, usaili na hojaji. Sura ya tano imewasilisha matokeo ya utafiti. Yanaonesha kuwa uhai wa fasihi ya Lugha unategemea ufundi na umakini wa mpangilio wa maneno. Kiini ikiwa ni dhima ya ufutuhi ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Kutokana na kukua kwa lugha ya Kiswahili na uwanda wake mpana wa fasihi imeonesha wazi kuwa, Dhima ya ufutuhi ni muhimu sana katika fasihi ili kuamsha ari na kuleta mvuto wa Lugha ya Kiswahili hususani katika kizazi hiki kilichopo. Hatimaye ni hitimishi na mapendekezo yaliyotolewa kama vile kuhimiza misingi bora ya ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili, mbinu shirikishi za dhima ya ufutuhi kulingana na wakati uliopo na kuhamasisha jamii na Taifa letu kuipenda na kuithamini lugha ya Kiswahili kama Lugha ya Taifa. Kusoma vitabu vyake Shaaban Robert, kuzuru maeneo ya asili yake na kuviingiza vitabu vyake katika mtalaa wa Elimu na somo la Kiswahili kwa ngazi zinazohusika.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 11 Jan 2016 14:25
Last Modified: 11 Jan 2016 14:25
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/874

Actions (login required)

View Item View Item