Kabeja, Fortunata Moses
(2013)
Dhima ya Ufutuhi Katika Riwaya za Shaabani Robert.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii imejaribu kuchangia mawazo na fikra za jinsi ya kutumia fasihi ya lugha
katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa kupitiya fani ya ufutuhi. Dhima ya ufutuhi
katika Riwaya za Shaaban Robert imeathiri wasomaji, watunzi na wapenzi wa lugha
ya Kiswahili kwa kiwango cha juu sana. Sura ya kwanza inatoa utangulizi wa ujumla
historia ya marehemu Shaaban Robert, maisha yake, familia yake, kazi na ajira zake,
mbari zake kwa ujumla na kazi zake za fasihi alizofanya. Sura ya pili inaelezea
mawanda yakinadharia, mkabala wakinadharia ambao umetoa mchango katika kazi
hii yaani nadharia tete na nadharia kiongozi. Sura ya tatu ni tahakiki za kazi
mbalimbali zilizotangulia ikielezea kazi mbalimbali kuhusu ufutuhi na Dhima ya
ufutuhi pamoja na maudhui yake katika Riwaya zilizo lengwa. Sura ya nne
inafafanua mbinu za utafiti ambazo zimetumika ikiwa ni pamoja na umakinifu, usaili
na hojaji. Sura ya tano imewasilisha matokeo ya utafiti. Yanaonesha kuwa uhai wa
fasihi ya Lugha unategemea ufundi na umakini wa mpangilio wa maneno. Kiini
ikiwa ni dhima ya ufutuhi ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Kutokana na kukua
kwa lugha ya Kiswahili na uwanda wake mpana wa fasihi imeonesha wazi kuwa,
Dhima ya ufutuhi ni muhimu sana katika fasihi ili kuamsha ari na kuleta mvuto wa
Lugha ya Kiswahili hususani katika kizazi hiki kilichopo. Hatimaye ni hitimishi na
mapendekezo yaliyotolewa kama vile kuhimiza misingi bora ya ufundishaji wa
Lugha ya Kiswahili, mbinu shirikishi za dhima ya ufutuhi kulingana na wakati
uliopo na kuhamasisha jamii na Taifa letu kuipenda na kuithamini lugha ya
Kiswahili kama Lugha ya Taifa. Kusoma vitabu vyake Shaaban Robert, kuzuru
maeneo ya asili yake na kuviingiza vitabu vyake katika mtalaa wa Elimu na somo la
Kiswahili kwa ngazi zinazohusika.
Actions (login required)
|
View Item |