Kufanana na Kutafautiana kwa Maudhui na Fani kati ya Methali za Kitanzania na za Kilibya: Utafiti Linganishi

El-Jetlawiy, Hamza Mansour Khalifa (2013) Kufanana na Kutafautiana kwa Maudhui na Fani kati ya Methali za Kitanzania na za Kilibya: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_HAMZA_-_FINAL_1.pdf]
Preview
PDF
Download (878kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulihusu Kufanana na kutofautiana kwa maudhui na fani kati ya methali za Kitanzania na Kilibya: Utafiti linganishi. Kwa msingi huo basi, lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza kufafana na kutofautiana kwa maudhui na kwa uchache fani kati ya methali za Kiswahili na zile za Kilibya. Ili kutimiza lengo hili madhumuni mahususi yalikamilishwa. Madhumuni hayo ni Kukusanya methali za Kiswahili na Kilibya na kuzianisha katika makundi, kuchunguza kufanana na kutofautiana kidhamira na kifani kati ya methali za Kilibya na Kiswahili na kuzichambua methali zote hizi ili kupata suluhu ya tatizo la utafiti. Katika kutimiza malengo haya mbinu za ukusanyaji wa data za maktabani na maskanini zilitumika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, methali za Kiswahili na za Kilibya zinafanana katika dhamira za elimu, malezi, maonyo, ushauri, kujali chako na udugu. Tofauti inaonekana pale ambapo methali za Kiswahili zinasisitiza zaidi juu ya umoja na udugu huku zile za Kilibya zikisisitiza zaidi juu ya kujali chako. Kwa upande wa fani tumebaini kwamba, methali za jamii hizi zinafanana katika kutoa msisitizo bayana, takriri dufu na vina. Kwa upande wa tofauti za kifani methali hizi zinatofautiana katika mtindo wa kishairi. Vile vile, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba sababu za kufanana kidhamira ni misafara ya biashara na nchi zote zipo katika bara la Afrika. Pia, sababu za kutofautiana ni tofauti za kilugha pamoja na mazingira baina ya jamii hizi mbili. Mwishoni mwa utafiti huu kumetolewa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 11 Jan 2016 14:29
Last Modified: 11 Jan 2016 14:29
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/871

Actions (login required)

View Item View Item