Kutathmini nyimbo katika kukuza na kuimarisha malezi,mfano wa kabila la Wakaguru

Kutamika, Silau Gervas (2013) Kutathmini nyimbo katika kukuza na kuimarisha malezi,mfano wa kabila la Wakaguru. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of DHIMA_YA_NYIMBO_ZA_NGOMA_-_1.pdf]
Preview
PDF
Download (3MB) | Preview

Abstract

Makusudi ya kufanya utafiti huu, ni kutathmini dhima ya nyimbo katika kukuza nakuimarisha Malezi,mfano wa kabila la Wakaguru,Utafiti huu umefanyika Wilayani Kilosa,kata za mbili za Rubeho na Chagongwe zilizopo wilaya mpya ya Gairo,Aidha kata zote mbili zimeshirikishwa kikamilivu, zikiwa maskani ya utafiti huu,Nyimbo za ngoma tatu zimetumika katika mchakato wa utafiti hadi kufukia Matokeo halisi ya utafiti.Ngoma zilzojumuishwa kwenye utafiti huu ni pamoja na Ngoma ya Digubi,Ngoma ya Jando na Ngoma ya Mtunya Zilichunguzwa dhima zao na umuhimu wao kwa jamii ya Wakaguru wenyewe na Taifa kwa ujumla wake.Njia zilizotumika katika kufikia ukamilifu wa kazi hii, zilikuwa ni utafiti wa Maktaba na ule wa ana kwa ana. Matokeo ya utafiti huu yamebaini yaufuatayo:Washiriki walioteuliwa ni 340 walifikiwa na kufanikisha utafiti. 1.Vijana wenye umri wa miaka kuanzia 11-18 hawashiriki kabisa katika shughuli nyimbo za jadi wamezamia katika kuufukuza utandawazi. 2.Asilimia 75 ya Walioteuliwa kwenye utafiti huu na wenye umri wa miaka 19-25 walishiriki katika shughuli za nyimbo za ngoma. Zipo nadharia kadhaa zililyotumika katika Tasnifu hii, kuhusu uwasilishaji na uchanganuzi wa takwimu,Nadharia hizo ni Nadharia ya fasihi ina kwao, Nadharia ya uhalisia na Nadharia ya Mtu na fasihi na Nadharia ya Dini ni Bangi, Tasnifu hii imeundwa na sura sita, ya kwanza inahusu utangulizi kwa ujumla, usuli wa tatizo umewekwa bayana .Dhana ya mwingiliano wa nyimbo za ngoma imejadiliwa kwa kuhusishwa na mwingiliano uliopo kati ya nyimbo za ngoma na utamaduni wa magharibi, unaovinjari Mithili ya kasi mawimbi ya vumbi,linalonyemelea kuumeza x utamaduni wa mwafrika, hususan katika eneo la kata za Rubeho na Chagongwe, ambako utafiti huu ndiko unakofanyika, ukiwakilisha maeneo yote yanayokumbwa na tamaduni za magharibi, ambazo tayari zimeleta athari kubwa ya kuporomoka kwa maadili ya jamii, kwani nyimbo za ngoma katika jamii zetu hasa Digubi, kwa ajili ya kuwafundisha na kuwataarisha watoto wa kike, katika kuyakabiri maisha yao ya ujana kwenda utu uzima na Jando lililotumika pia kuwaandaa vijana wakiume kwa maisha mema na kupata mwongozo im arawa maisha yao ya jamii,na jamii zinazowazunguka. Pamoja na usuli wa tatizo sura hii imeonesha waziwazi malengo ya utafiti huu. sura ya pili inahusu nadharia na mbinu zilizotumika katika utafiti huu, katika sura hii.Dhana ya nadharia imeelezwa ,Aina za nadharia zimeelezwa, na nadharia zilizotumika kwenye utafiti huu, zimebainishwa, aidha eneo la utafiti, wahusika lengwa, namna ya ukusanyaji wa takwimu, muundo wa ukusanyaji wa takwimu, mpango wa uchanganuzi wa takwimu, katika utafiti; vyote hivyo vimefafanuliwa wazi kuhusu zana zilizotumika,utafiti huu umetumia uchunguzi wa maktaba, masaili na maswali ya dodoso. Sura ya tatu imeshughulikia mapitio mbalimbali ya maandishi yanayohusu Fasihi ya ngoma ,Jando, na Digubi,katika sura hii imetoa maana na dhanna nzima ya ngoma, jando, digubi,Fasihi ya ngoma na nyimbo za ngoma vimeelezwa na kufafanuliwa kwa kina.Dhanna za maadili,malezi navyo vimejadiliwa. Sura ya nne imehusika na mambo makuu mawili ;Mbinu na njia za kukusanya data,uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Wahojiwa waliotarajiwa walikuwa 1,720,000 lakini waliofanikiwa kufikiwa walikuwa 340 na ndio walioleta matokeo xi halisi ya utafiti,kwa hiyo uwasilishaji na uchanganuzi wa takwimu hizo umetumia takribani robo idadi kuu watu katika kata hizo.Orodha ya wahojiwa imeambatanishwa nyuma ya taarifa hii, kama kiambatanishi A na E kinabainisha. sura hii imebainisha wazi uhusiano uliokuwapo hapo zamani, kati ya tabia njema kwa vijana na mafunzo yaliyotokana na nyimbo za ngoma za digubi na jando. Sura ya tano imejadili nadharia ya fasihi inakwao,Nadharia ya uhalisiya na Nadharia ya udhanaishi,Nadharia ya Ufeministi, Nadharia ya dini ni bangi,Nadharia ya ujumi na Nadharia ya ndani nje katika kuhakiki vipengele vya fani na maudhui ya kazi yote,hizi zimefafanuliwa kwa kina na kwa kuzingatia nadharia saidizi tatu za nadharia ya fasihi inakwao,Nadharia ya uhalisiya na Nadharia ya udhanaishi, Na hatimaye muhtasari wa utafiti,hitimishi yake na mapendekezo kadhaa, kwa ajili ya tafiti zaidi vimetolewa katika sura hii,imejadili nadharia ya fasihi inakwao,Nadharia ya uhalisiya na Nadharia ya udhanaishi,

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 11 Jan 2016 14:56
Last Modified: 11 Jan 2016 14:56
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/863

Actions (login required)

View Item View Item