Usawiri wa Jinsia Katika Lugha ya Mashairi: Mifano kutoka Mashairi ya Shaaban Robert

Salem, Badredden Mohamed (2013) Usawiri wa Jinsia Katika Lugha ya Mashairi: Mifano kutoka Mashairi ya Shaaban Robert. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of BADRE-AFTER_VIVA_FINAL-2.pdf]
Preview
PDF
Download (828kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu Usawiri wa Jinsia Katika Lugha ya Mashairi: mifano kutoka katika mashairi ya Shaaban Robert. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza usawiri wa jinsia katika lugha ya mashairi ya Shaaban Robert katika kazi zake za fasihi za Pambo la Lugha na Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini ili kuonyesha jinsi lugha inavyotumika kujadili suala la ujinsia. Utafiti huu ulitumia mbinu nne za ukusanyaji data ambazo ni; maktaba, usaili, dodoso na majadiliano ya vikundi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya; madhumuni maalum, kimfumo na uteuzi wa nasibu takabishi. Utafiti huu umegundua kuwa, tamathali za semi zilizotumika katika mashairi ya Shaaban Robert ni: Sitiari, takriri, tashihisi, tasifida na tashibiha. Aidha utafiti huu uligundua kuwa tamathali za semi husawiri swala la ujinsia kwa kuonyesha mahusiano tofauti baina ya mwanamke na mwanaume. Kwa kutumika tamathali za semi mwanamke husawiriwa kama kiumbe dhaifu, tegemezi na asiye na maamuzi binafsi ukilinganisha mwanaume ambaye huonekana kuwa ni jasiri, hodari, shupavu na mwenye maamuzi binafsi. Vile vile, utafiti huu uligundua kuwa, matumizi ya tamathali za semi husawiri nafasi ya mwanamke katika jamii. Kwa kutumika tamathali za semi nafasi ya mwanamke inajibainisha katika: mwanamke katika asasi ya ndoa, mwanamke katika kufanya maamuzi, mwanamke katika elimu, mwanamke katika uzazi na malezi, mwanamke katika mapenzi, mwanamke katika utamaduni, mwanamke katika dini na mwanamke kama kiumbe muhimu katika jamii.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Jan 2016 12:00
Last Modified: 14 Jan 2016 12:00
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/843

Actions (login required)

View Item View Item