Kuchunguza Jinsi Methali za Kiswahili Zinavyosawiri Suala la Mapenzi na Ndoa Visiwani Zanzibar

Makame , Ahmed Ali (2013) Kuchunguza Jinsi Methali za Kiswahili Zinavyosawiri Suala la Mapenzi na Ndoa Visiwani Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Tasnifu.doc] PDF - Submitted Version
Download (517kB)

Abstract

Methali ni moja kati ya vipengele vya semi ambavyo hutumika sana katika masuala yanayohusu mapenzi na ndoa. Mara nyingi mtu huweza kuwasikia wanawake wakipigana mafumbo wanapokwenda visimani, maharusini na hata wanapokwenda matangani. Mara nyenginemafumbo hayo hayajidhihirishi wazi wazi bali vifaa kama vile kanga, makawa, mikoba na mfano wa hayo, hutumika katika kufikisha ujumbe Fulani kuhusiana na msuala hayo ya mapenzi na ndoa. Mbali na upande wa mapenzi na ndoa, methali hutumiwa pia katika kutoa utangulizi na uhitimishi wa maongezi Fulani hasa yale yanayohusu kuwakanya vijana. Kutokana na matumizi hayo makubwa ya methali, mtafiti aliingia hamu ya kutaka kuelewa kwa namna gani methali za Kiswahili zinasawiri masuala ya mapenzi na ndoa za Wazanzibari. Utafiti huu ulifanyika katika wilaya ya mjini, Shehia ya Kiembe Samaki katika Mtaa wa Mombasa visiwani Zanzibar. Watu kadhaa walipata kuhojiwa kuhusiana na masuala ya methali, waswahili na ndoa zao. Miongoni mwa watu hao, ni pamoja na makungwi na masomo. Pamoja na kuchukua hadhari kubwa katika kutoa majibu ya maswali waliyoulizwa na mtafiti katika hatua za awali za mahojiano, kazi ya mahojiano ilipoendelea, watafitiwa hao waliweza kutoa maelezoyaliyomsaidia sana mtafiti katika kuyakamilisha madhumuni yake. Mbinu mbali mbali zimetumika katika utafiti huu ikiwa ni pamoja na ile ya kuzitumia hojaji, mbinu ya usaili pamoja na mbinu ya kuzitumia maktaba. Katika kufafanua matokeo ya utafiti, majedwali mbali mbali yametumika. Utafiti huu, mbali ya kusaidia katika suala la marejeleo ya kazi za kifasihi bali pia utawasaidia wanandoa kuzifanya ndoa zao kuwa imara zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Jan 2016 12:02
Last Modified: 17 Oct 2018 14:53
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/828

Actions (login required)

View Item View Item