Massoud, Salem Mahmoud Abdulhadi
(2013)
Maudhui na Fani Katika Tamthilia za Kiswahili: Utafiti Linganishi wa Tamthilia za Mashetani na Kivuli Kinaishi.
["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu maudhui na fani katika tamthilia za kiswahili ambao umetumia mifano ya tamthilia ya Mashetani na Kivuli Kinaishi. Utafiti huu ni utafiti linganishi ambao ulilenga kuchunguza mtindo wa kimaudhui na kifani katika tamthilia ya Mashetani na Kivuli Kinaishi ili kuona ni jinsi gani msanii anaweza kutofautiana ama kufanana na msanii mwingine katika uteuzi na utumizi wa vipengele vya kimtindo. Utafiti huu ulitumia mbinu nne za ukusanyaji data ambazo ni; maktaba, usaili, dodoso na majadiliano ya vikundi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalum, bahatishi na uteuzi rahisi. Aidha data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui na uchambuzi linganishi. Utafiti huu uliongozwa na Nadhariatete ya Elimumitindo katika Uchambuzi wa Matini za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwa, msanii wa Mashetani na msanii wa Kivuli Kinaishi wanatofautiana na kufanana katika mbinu za kimtindo ambazo wametumia kujenga kazi zao za sanaa. Matokeo haya yanaendana na nadharia ya mtindo na mazingira kuwa wasanii hutofautiana katika uteuzi wa mbinu za kimtindo kutokana na tofauti za kimazingira, kihistoria, kijiografia na kimuktadha. Utafiti huu umegundua kuwa, wasanii wote wanafanana katika maudhui ambayo wameyaibua katika kazi zao. Utafiti unajadili kuwa pamoja na kuwa wametofautiana katika mazingira ya kijiografia, lakini wanatoka katika jamii zinazofanana kihistoria, kiitikadi, kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kukaribiana sana kiutamaduni. Hivyo basi, ni dhahiri kuwa jamii zote hizi zina matatizo, mahitaji na matarajio yaliyo sawa ambayo watunzi wanayashughulikia.
Actions (login required)
|
View Item |