Masuala ya Kisiasa Katika Ushairi wa Kandoro: Mifano Kutoka Katika Mashairi Yake

Yunus, Mohamed Khalfan (2013) Masuala ya Kisiasa Katika Ushairi wa Kandoro: Mifano Kutoka Katika Mashairi Yake. ["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Masuala_ya_Kisiasa_katika_ushairi_wa_Kandoro.pdf]
Preview
PDF
Download (849kB) | Preview

Abstract

Nia kuu ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza masuala ya kisiasa katika ushairi wa Kandoro kwa kutolea mifano mashairi yake. Nia hii kuu imeweza kufanikiwa kutokana na kukamilika kwa madhumuni mahususi matatu ambayo ni: kuainisha dhamira za kisiasa zinazojitokeza katika ushairi wa Kandoro, kueleza mbinu za kisanaa zinazotumiwa na Kandoro katika kuibua masuala ya kisiasa na kubainisha falsafa ya Kandoro kama inavyojitokeza katika ushairi wake. Ili kuwezesha malengo haya kukamilika tumefanya mapitio ya kazi tangulizi zinaohusiana na mada ya utafiti, tumeainisha nadharia zilizoongoza utafiti wetu na baadaye kuainisha mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, Kandoro anaeleza dhamira za kisiasa zinazohusiana na ukombozi wa Mwafrika kutoka katika mikono ya wakoloni na kuweza kujitawala mwenyewe. Ili kufanikisha jambo hili Kandoro anawataka wananchi kuungana pamoja katika kudai uhuru wao. Aliwataka kufanya hivyo kwa kujiunga na chama cha TANU ili kukipa nguvu ya ushindi dhidi ya wakoloni. Baada ya kupatikana kwa uhuru Kandoro aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo endelevu. Kazi kubwa aliyoihimiza bwana Kandoro ni kilimo ambacho kilitamkwa kuwa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa taifa na hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Matokeo ya utafiti yanaonesha pia kuwa, dhamira hizi za kisiasa zimeweza kuwafikia wasomaji kutokana na matumizi mbalimbali ya mbinu za kisanaa kama vile matumizi ya lugha ya kitamathali, wahusika, muundo, mtindo na kadhalika katika mashairi ya Kandoro. Vilevile, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, Kandoro ana falsafa ya kimapinduzi, utu, ujamaa na kujitegemea. Mwishoni mwa utafiti huu tumetoa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazo

Item Type: Thesis (["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined])
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Jan 2016 12:04
Last Modified: 14 Jan 2016 12:04
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/809

Actions (login required)

View Item View Item