Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano Kutoka Kuli na Vuta N’kuvute

Adam, Omar Abdalla (2014) Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano Kutoka Kuli na Vuta N’kuvute. ["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of THESIS_-_OMAR_ADAM_MPYA_LEO.docx] Microsoft Word
Download (299kB)

Abstract

Riwaya za Kuli na Vuta N’kuvute zimepata umaarufu na kuwa riwaya nzuri na imara za mtunzi Shafi Adam Shafi. Utafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza dhamira za kijamii na kiutamaduni zinazojitokeza katika riwaya hizo mbili (Kuli na Vuta N’kuvute). Katika kutimiza nia hii, tulikusanya data kwa kutumia mbinu za maktabani, mahojiano ya ana kwa ana kufanya na uchambuzi wa kimaudhui. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutumia mbinu za mkabala wa kimaelezo na ule wa kidhamira. Nadharia za Simiotiki, Saikolojia Changanuzi na dhima na kazi, ndizo zilizotumika katika kuhakiki riwaya hizo mbili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, dhamira zinazojitokeza zaidi katika riwaya hizo mbili ni matabaka katika jamii, ndoa za kulazimishwa, mapenzi na ukarimu katika riwaya ya Vuta N’kuvute. Katika Kuli, dhamira zinazojitokeza zaidi ni busara na hekima, umuhimu wa elimu, umasikini, utamaduni na mabadiliko yake, ukombozi katika jamii na masuala ya uzazi. Dhamira hizo zimesheheni uhalisia katika maisha ya sasa ya jamii ya leo. Pia matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, mbinu za kisanaa zinazotumiwa na mtunzi katika uwasilishaji wake wa dhamira ni upambaji wa wahusika, usimulizi, kuingiliana kwa tanzu, tashibiha, misemo, takriri, taswira, motifu na matumizi ya barua.

Item Type: Thesis (["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined])
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Jan 2016 12:11
Last Modified: 14 Jan 2016 12:11
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/738

Actions (login required)

View Item View Item