Mapunjo, George Cleopa
(2014)
Usawiri wa Mwanamke Kama Kiongozi Katika Tamthiliya: Uchunguzi wa Kivuli Kinaishi na Nguzo Mama.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Kazi hii ilichunguza dhima ya usawiri wa mwanamke kama kiongozi katika tamthiliya: Uchunguzi wa Kivuli kinaishi na Nguzo mama. Lengo la jumla ya utafiti huu ilikuwa kutafiti na kubainisha usawiri wa mwanamke kama kiongozi na kuonesha suala la uongozi linavyoibua visa na linavyojenga dhamira katika tamthiliya teule. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu ya maktabani katika kukusanya na kuwasilisha data kimaelezo. Vilevile marejeleo mbalimbali kutoka katika wavuti yalipitiwa. Nadharia ya U-feministi ndiyo iliyotumika katika kufanikisha utafiti huu. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuweza kubaini mawazo mbalimbali ya waandishi katika riwaya zao ambazo ni aina za uongozi, visa na maudhui yanayotokana na uongozi kutoka katika tamthiliya ya Kivuli Kinaishi na Nguzo Mama. Kwa ujumla matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti kwani yalibainisha uongozi ulivyo na dhamira zake katika jamii. Dhamira hizo ni uvivu, ushirikina, ushirikiano na suala zima la mapinduzi ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi. Pia matokeo hayo ya utafiti yalibainisha mnyonge kumshinda mwenye nguvu, utundu na ubunifu. Matokeo mengine ni umalaya, mauaji ya wenye kudai haki, ulevi, tamaa ya binadamu na ndoto za kutawala milele. Dhamira zinazotokana na suala la uongozi kutoka katika tamthiliya ya Kivuli Kinaishi na Nguzo Mama yana mchango mkubwa katika fasihi kwa ujumla.
Actions (login required)
|
View Item |