Uchunguzi wa Mtindo katika kasida za Dufu za Kiislamu.

Sheha, Mwanakombo Mwadini (2025) Uchunguzi wa Mtindo katika kasida za Dufu za Kiislamu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA MWANAKOMBO MWADINI SHEHA MPYA ILIYOSETIWA.doc] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (2MB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Utafiti huu ulichunguza “Uchunguzi wa Mtindo ya Kasida za Dufu za Kiislamu”. Mtafiti aliongozwa na malengo mahsusi matatu nayo ni Kufafanua mitindo ya kasida za dufu za Kiiislamu katika madrasa teule, Kuchambua mitindo ya kasida za dufu za Kiislamu iliyojitokeza katika kasida teule na Kubainisha namna mitindo ya kasida ya Kiislamu ilivyoibua dhamira. Malengo haya yaliukamilisha utafiti hatua kwa hatua katika kugundua mitindo ya kasida za dufu za Kiislamu. Mtafiti alikusanya data kupitia nyanjani katika madrasa tafauti zilizopo wilaya ya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Mtafiti aliwagawa watafitiwa katika makundi ya watunzi, walimu na wanafunzi. Kwa upande wa ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti mtafiti aliongozwa na nadharia ya Mwitiko wa Msomaji, Upokezi na Umitindo. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamethibitisha kuwapo kwa mitindo ya kasida za dufu za Kiislamu katika madrasa teule ambayo ni mtindo wa Ajmi, Bayati, Sika/Hijazi, Razdi/rasti, Muundo wa neno moja, mtindo wa mshangao, mtindo wa takriri, mtindo wa kutumia nafsi kwanza, ya pili, umoja ya pili wingi, na nafsi ya tatu umoja. Pia utafiti uligundua kuwapo kwa mtindo wa matumizi ya lugha ya tash-biha, sitiari, tash-hisi, taswira, tanakalisauti, mdokezo, nidaa, tafsida, hutuba na swali. Dhamira zilizoibuliwa na mtindo katika kasida ni zile za kijamii, kimapenzi, utukufu, upekee, majonzi, ukiwa, wasifu, mwitiko, ushajihisho, unyenyekevu, nasaha, kukumbushana, hamasa, ushawishi, kujikubalisha, kujimithilisha, uthibitisho na usaili. Mwisho, utafiti umependekeza watunzi wa kasida za dufu waendelee kutunga kasida nyingine zenye maudhui mbalimbali ili watafiti waweze kuibua mitindo, mbalimbali itakayokuza na kuendeleza fasihi ya Kiswahili.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Jan 2026 15:18
Last Modified: 30 Jan 2026 15:18
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/5009

Actions (login required)

View Item View Item