Haji, Ilyas Nassib
(2025)
Falsafa za Nyimbo za Harusi za Kimakunduchi katika kudumisha Ndoa.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Wamakunduchi wanatumia Nyimbo za harusi kama njia ya kuwafunda wanandoa wao. Nyimbo hizo zinakuwa na msaada mkubwa katika mila na desturi walizojiwekea katika kudumisha ndoa. Mtafiti amefanya utafiti kwa lengo la kuchunguza falsafa za nyimbo za harusi za Kimakunduchi katika kudumisha ndoa, katika Shehia tatu ambazo ni Kiongoni, Kajengwa na Ng’anani. Watoa taarifa walikuwa ni wakaazi wa Makunduchi. Utafiti ulikusanya data kwa mbinu ya Usaili wa nusu kimuundo (Semi Structured Interview) na kupitia Machapisho. Nadharia ya uhalisia imetumika katika utafiti huu kutokana na kuonyesha uhalisia wa maisha jinsi yalivyo kulingana na falsafa zinazoibuliwa kupitia Nyimbo hizo zikiwa na lengo kuu la kudumisha ndoa. Data zilizokusanywa ni zile zinazozungumzia Maadili, nidhamu, suala la unyumba, kujenga udugu katika familia na kukemea maovu katika ndoa. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha wazi kuwa nyimbo za harusi zina falsafa kubwa ya kudumisha ndoa kwa wanajamii wa Makunduchi na Watanzania kwa ujumla.
Actions (login required)
 |
View Item |