Juma, Rukia Msago
(2025)
Athari ya Lugha ya Kiha katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii ina lengo la kuona athari ya lugha ya Kiha katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za msingi na sekondari wilayani Kasulu. Utafiti huu una malengo mbalimbali. lengo kuu ni kuchunguza athari ya Kiha katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Pia, malengo mahususi ni kuainisha athari hasi na chanya za lugha ya Kiha, pili, kuainisha sababu mbalimbali za lugha ya Kiha kuathirhi ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na kutafuta njia za kutatua athari zinazopelekea lugha ya Kiha kuathiri lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umetumia nadharia ya mawasiliano. Nadharia hii ina lengo la kukuza na kuweka mikakati mizuri kwa wale wanaojifunza lugha ya pili. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Kigoma, taasisi mbili, shule za msingi na shule za sekondari, wakiwemo walimu na wanafunzi na wanakijiji wa kijiji cha Lusesa. Utafiti huu utatumia mbinu za utafiti ambazo ni hojaji, mahojiano na majadiliano ya makundi katika kukusanya takwimu. Utafiti lina jumla ya watafitiwa 45 miongoni mwao wakiwa walimu 10, wanafunzi wa sekondari 10, wanafuzi wa msingi 10 na wanajamii 15 ambao watatusaidia kukusanya takwimu, mapendekezo ya mtafiti ni kwamba lugha ya Kiha inaleta athari kwa watu wa lugha Kiha wanapokuwa wanajifunza lugha ya Kiswahili sanifu. Hivyo, ipo haja ya kuanza kujifunza lugha ya Kiswaili mazingira yote
Actions (login required)
 |
View Item |