Usarufi wa Mandhari Lugha ya Kiswahili katika Maandishi ya Bajaji za Jijini Mwanza.

Maige, Benjamine (2023) Usarufi wa Mandhari Lugha ya Kiswahili katika Maandishi ya Bajaji za Jijini Mwanza. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI BENJAMINI MAIGE.doc] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (4MB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Utafiti huu ulichunguza usarufi wa mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza. Utafiti umefanyika mkoa wa Mwanza, wilaya ya Nyamagana katika kata za Buhongwa, Mkolani, Nyegezi, Butimba, Mahina, Nyakato, Kishiri na Igoma. Utafiti huu una malengo mahususi matatu, nayo ni kufafanua maana za mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza, kuchunguza maumbo ya maneno ya mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza na kuchunguza mpangilio wa maneno katika mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya muktadha kama mwongozo wa kufasili maana za maneno kulingana na miktadha ya matumizi ya lugha na nadharia ya sarufi miundo virai kama msingi mkuu katika kutafiti sarufi miundo na sarufi maumbo. Jumla ya picha 80 za mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza zilipigwa na kufanyiwa utafiti kwa mujibu wa malengo mahususi ya utafiti huu. Aidha, watafitiwa 80 ambao ni madereva bajaji husika walishirikishwa katika upatikanaji wa data za utafiti. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji usionasibu kusudio na usampulishaji usionasibu fursa. Data zilichambuliwa kwa mujibu wa mkabala wa kimaelezo pamoja na mkabala wa kiidadi kwa kigezo cha kimaudhui. Data za utafiti zilikusanywa kwa njia ya mahojiano, ushuhudiaji na upigaji picha. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa maana za mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza yamebainishwa katika miktadha ya kijamii, kiisimu, kiusemi, ushawishi na mtindo. Maumbo ya maneno yameainishwa katika kategoria za mofu ambazo ni mofu huru, mofu tegemezi, mofu tata na mofu changamano. Vilevile mpangilio wa maneno katika mandharilugha ya Kiswahili katika maandishi ya bajaji za jijini Mwanza umebainishwa katika kigezo cha mpangilio sahihi wa maneno, udondoshi wa sauti, udondoshi wa viunganishi, udondoshi wa vitenzi, makosa katika upatanisho wa kisarufi, utenganishi wa nomino ambatani, makosa ya kitahajia na ukiukwaji wa kanuni za uandishi. Hata hivyo, utafiti huu umependekeza watafiti wengine wachunguze usarufi wa mandharilugha ya Kiswahili katika maeneo mengine ya wazi, ya kuonwa na watu kama vile kandokando ya barabara za umma na mbele ya maduka.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Aug 2025 13:55
Last Modified: 29 Aug 2025 13:55
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4514

Actions (login required)

View Item View Item