Kuchunguza Dhamira Zilizojengwa Kupitia Tashititi katika Tamthilia za Kitanzania na Kimisri.

Gohar, Abdallah Masoud Saad Ahmad (2023) Kuchunguza Dhamira Zilizojengwa Kupitia Tashititi katika Tamthilia za Kitanzania na Kimisri. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ABDALLAH MASOUD SAAD AHMAD.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulihusu kuchunguza dhamira kupitia tashititi kwa kurejelea tamthilia teule za nchini Tanzania na Misri. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa mawili na lengo la kwanza lilihusu kuchambua dhamira zinazotokana na matumizi ya tashititi katika tamthilia teule. Lengo la pili lilihusu kuonesha kufanana na kutofautiana kwa dhamira zinazotokana na matumizi ya tashititi katika tamthilia teule (tamthilia teule za Kaptula la Marx iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi na Embe Dodo iliyoandikwa na Dominicus Makukula ambazo ni za watunzi wa Kitanzania na Bwana Wetu Al-Muqadam (مولانا المقدم) iliyoandikwa na Walid Alaaeldin na Wananchi Wanapotoroka (الشعب لما يفلسع) iliyoandikwa na Mahmoud Altokhy za watunzi wa Misiri). Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Nadharia ya Fasihi Linganishi, Simiotiki na Usosholojia zimetumika katika uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Matokeo ya utafiti yanabainisha kwamba matumizi ya tashititi katika tamthilia teule yamesaidia kujenga na kuibua dhamira mbalimbali. Baadhi ya dhamira hizo zinahusu masuala ya ujamaa, ukosefu wa usawa, ufisadi, ukoloni mamboleo, matumizi mabaya ya madaraka, ukosefu wa demokrasia, ubaguzi wa kijinsia, nafasi duni ya mwanamke na malezi ya watoto. Tasinifu hii imeshughulikia suala la tashititi kwenye tamthilia ya Kitanzania na ya Kimisri. Tunapendekeza kufanya utafiti zaidi kuhusu Fasihi Linganishi baina ya tanzu za fasihi ya Kitanzania na ya Kimisri. Maneno Muhimu: Tashtiti, Tamthilia, Fasihi Linganishi

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 28 Oct 2024 11:47
Last Modified: 28 Oct 2024 11:47
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4412

Actions (login required)

View Item View Item