Makame, Khatib Haji
(2023)
Kuchunguza Dhamira Vuate zinazoibukakatika Methaliza Kipembana.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulilenga “Kuchunguza Dhamira Vuate zinazoibuka katika Methali za Kipemba.” Utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandani katika ukusanyaji wa data. Maeneo yaliyotumika kukusanya data ni katika shule za sekondari za Vitongoji, Dkt. Omar, Utaani na Mchangamdogo. Maeneo haya yalitumika kukusanya data kwa kutumia hojaji. Maeneo mengine yaliyotumika kupata data za Mahojiano ni Wawi na Vitongoji. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalum. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Nadharia ya Simiotiki. Jumla ya Methali thelathini na tano za jamii ya Wapemba zilichambuliwa kutoka kwa watafitiwa waliojaza dodoso na wale waliohojiwa kwenye eneo la utafiti. Data zilifanyiwa uchambuzi na uwasilishaji kwa njia ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi mawili ambayo ni; “Kubainisha methali mahususi za jamii ya Wapemba.” Lengo hili liliongozwa na swali la utafiti lisemalo “Ni methali zipi mahususi za jamii ya Wapemba?” Lengo mahsusi la pili la utafiti huu lilikuwa ni: “Kubainisha Dhamira Vuate zinzojitokeza katika methali za jamii ya Wapemba”. Lengo hili liliongozwa na swali la utafiti lisemalo “Ni dhamira zipi zilizovuatwa katika methali za jamii ya Wapemba?” Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, methali za Kipemba hugawanyika kwenye matapo mbalimbali. Zipo methali zinazohusu Nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiaza, kimapenzi na hata kiutamaduni. Baadhi ya methali za Kipemba huvuata dhamira moja na nyengine huvuata dhamira zaidi ya moja.
Maneno Makuu:Kuvuata, Kipemba, Dhamira
Actions (login required)
|
View Item |