Mwacha, Monica Remi
(2023)
Tathmini Ya Athari za Lugha ya Kibosho katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili: Mifano kutoka Wanafunzi wa Shule za Msingi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo la utafiti huu ni kutathmini “Athari ya Lugha ya Kibosho katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili: Kwa Kutumia Mifano kutoka kwa wanafunzi wa shule za msingi”. Malengo mahususi matatu ya utafiti ni; kwanza ni kubaini athari za kiisimu za lugha ya Kibosho katika kujifunza lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za msingi, pili lilikuwa ni kutathmini sababu zinazowasababisha wanafunzi wa Kibosho kama L1 kuathiriwa na lugha yao katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama L2 na tatu ni kuainisha mbinu za kipedagojia katika kusahihisha athari za wanafunzi wanaozunguma Kibosho kama L1 wakati wanajifunza Kiswahili kama L2. Nadharia iliyoongoza utafiti huu Uchanganuzi Linganuzi (UL) ambayo huchunguza athari ya L1 kwenye L2. Mbinu mbalimbali za utafiti zilitumika; piadata zilikusanywa katika Wilaya ya Moshi Vijijini katika shule za msingi za Masako, Boro, Kidachini na Kirima Juu. Watoa taarifa waliohusika ni wanafunzi na walimu wa shule hizo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu; hojaji, mahojiano na mbinu ya insha. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa lugha ya Kibosho imeathiri lugha ya Kiswahili hususani katika vipengele vya kimatamshi, kimsamiati na kimaana. Pia yameonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zilizochangia lugha ya Kiswahili kuathiriwa kama vile; uzoefu wa kutumia lugha mama na athari za matamshi katika lugha ya Kibosho. pia, mbinu za kipedagojia za kusahihisha athari hizo ni pamoja na walimu wawaelekeze wanafunzi utamkaji mzuri wa matamshi nayaandaliwe makongamano, warsha na mafunzo mbalimbali kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu unapendekeza watafiti wajao wafanyie utafiti juu ya athari za kimuundo za lugha ya Kibosho katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili
Actions (login required)
|
View Item |