Hussein, Khadija Abubakar
(2023)
Unominishaji na Utenzishaji wa Maneno ya Kiswahili katika Rejista za Magazetini.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umechunguza miundo ya unominishaji na utenzishaji katika gazeti la Zanzibar leo. Utafiti huu uliongozwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha maneno yaliyonominishwa na yaliyotenzishwa katika lugha ya Kiswahili na pili, kufafanua miundo ya maneno iliyotumika katika kunominisha na kutenzisha katika habari za kawaida na habari za michezo katika gazeti la Zanzibar Leo. Aidha, nadharia ya mofolojia, Leksika na usarufishaji zilitumika katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Data za utafiti huu zilikusanywa kupitia mbinu ya usomaji wa nyaraka za gazeti la Zanzibar leo . Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni orodha ya maneno yaliyochukuliwa na kuchunguzwa katika gazeti la Zanzibar leo. Jumla ya maneno ishirini na tano (25) yalibainika kuwa yamenominishwa ambayo ni sawa na asilimia 47 za maneno yote yaliyochunguzwa. Vilevile, maneno ishirini na sita (26) yalibainika kutenzishwa katika gazeti hilo, ambayo ni sawa na asilimia 53 ya maneno yote. Matokeo ya utafiti huu yameonesha miundo na viwango mbalimbali vya unominishaji na utenzishaji vimejitokeza katika gazeti la Zanzibar leo. Matokeo haya, yanathibitisha kuwa uandishi wa magazeti hutumia mbinu za usarufi katika kunominisha na kutenzisha. Ingawa wengi wao hawatumii miundo hiyo kwa taaluma bali hutumia kama ni mazoea katika matumizi ya lugha ya uandishi wa habari. Utafiti huu unapendekeza kufanyika tafiti zaidi kuhusu sarufi ya lugha hasa katika uandishi wa magazeti katika maeneo ya uchomozi wa virai namuundo wa uchanganyaji lugha na athari zake katika magazeti ya udaku, na ushikamani wa matini katika habari.
Actions (login required)
|
View Item |