Mulikuza, Paschal
(2023)
Athari za lugha ya Kisukuma katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili Sanifu.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo la tasnifu ni kutathmini athari za lugha ya Kisukuma Katika Kujifunza lugha ya Kiswahili sanifu kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, sababu za athari hizo na mbinu za kutatua athari hizo. Utafiti huu umefanywa katika mkoa wa Tabora, wilaya ya Tabora mjini katika Shule za msingi za Mwenge, Isike, Mihayo na Kitete. Utafiti huu umetumia nadharia ya Uchanganuzi Linganishi ambayo hutoa maelezo juu ya lugha ya kwanza na lugha ya pili ambapo kwa muktadha wa kazi hii ni lugha ya Kisukuma na Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu mbili za ukusanyaji data ambazo ni; hojaji na mahojiano. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu yenye madhumuni maalumu na mbinu bahatishi. Matokeo ya utafiti huu yanabainisha kuwa, athari za matamshi zinazojitokeza kwa wanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili. Athari hizo ni pamoja na udondoshaji wa sauti, kutumia sauti zinazokaribiana, athari za kimofolojia za lugha ya Kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili Sanifu. Data za utafiti huu zinathibitisha kuwa kuna athari za kimofolojia za lugha ya kisukuma ambazo pia zinajitokeza kwa wazungumzaji wa kisukuma wanaojifunza Kiswahili sanifu. Miongoni mwa athari zilizobainika ni kuongeza viambishi visivyohitajika katika maneno. Kiwango cha athari za kifonolojia na kimofolojia alizogundua mtafiti, ilihusisha matamshi, kuongeza viambishi ambavyo vilitokana katika lugha ya Kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili sanifu. Matokeo ya utafiti huu yanaweza kutumiwa na Taasisi ya ukuzaji mitaala kutoa mapendekezo kwa wanaojifunza Kiswahili kwa kuwashirikisha wanafunzi kimazungumzo kwa lengo la kuinua kiwango cha umilisi wa lugha. Hitimisho kwanza utafiti huu umeshughulikia athari za Lugha ya Kisukuma katika kujifunza Lugha ya Kiswahili sanifu, ni matarajio ya mtafiti kwamba, watafiti wengine wanaweza kufanya utafiti juu ya athari za lugha nyingine za Kibantu zinazotokana na tofauti za kisarufi baina ya lugha hizi mbili.
Actions (login required)
|
View Item |