Uchunguzi waSababu na Athari zaKutofautiana kwa Idadi ya Fonimu na Viashiria vyake katikaKiswahili Sanifu

Khamis, Amour A. (2024) Uchunguzi waSababu na Athari zaKutofautiana kwa Idadi ya Fonimu na Viashiria vyake katikaKiswahili Sanifu. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU SAHIHI YA AMOUR 5.docx] HTML - Submitted Version
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulichunguza sababuna athari za kutofautianakwa idadi ya fonimu na viashiria vyake katika Kiswahili sanifu. Uchunguzihuu ulifanyika kutokana na kuwagunduawataalamu zaidi ya 35 waliotofautiana katika uwasilishaji wao wa idadi ya fonimu na viashiria vyake katikaKiswahili sanifu. Utafitiuna malengo mahsusi ya kubaini sababu, athari na mapendekezo ya tatizo la kuofautiana kwa wataalamu katika uwasilishaji wa idadi ya fonimu na viashiria vyake katika Kiswahili sanifu. Utafiti ulitumianadhariaya Lyons (1968) yaUmbo-Sauti Maumbo Kimatumizipamoja na kanuni ya Trubetzkoy (1939/1969) ya Nitoe Nikutoe katika JoziSahili. Data zilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Sampuli ilikuwa na Wasailiwa115walioteuliwa kutoka vyuo vikuu vya SUZA, ZU, SU na MNMA. Data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya majedwali, grafu na maelezo.Utaftiulibaini kwamba, kutofautiana kwa idadi ya fonimu na viashiria vyake katika Kiswahili sanifu kuna sababu14na athari 15. Utafiti ulibaini sababu kuu ni ile ya wataalamu kutoainisha kanuni inayowasilisha idadi ya fonimu na atharikuu ni ile ya kuibuamgogoro wa kuwachanganya na kuwababaisha wahadhiri, wanataalumana wasomi wa vyuoni kwa kutojua idadi gani ni sahihi kati ya 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38, 40, 41, 42, 45 na 58. Utafiti pia uligundua kuwa kutofautianakwa idadi ya fonimu na viashiria vyake, kumetokana na wataaalamu zaidi ya 35 kuwasilisha baadhi ya fonimu ambatano ambazo hazikubaliki kuwa ni fonimu baada ya kupimwa kwa kanuni ya kisayansi inayowasilisha idadi sahihi ya fonimu na viashiria vyake.Utafiti umethibitisha kwamba, kanuni ya Nitoe Nikutoe katika Jozi Sahili za maneno ni ya kisayansi na ni suluhisho la kuwasilisha idadiya fonimu za Kiswahili sanifu. Kanuni hii itaweza kuziba pengo la kutofautianakwa idadi ya fonimu na viashiria vyake katika Kiswahili sanifu. Kwa kuondosha tatizo la kutofautiana, Utafitiulipendekeza wataalamu wa fonolojia ya Kiswahili sanifu wakiongozwa na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, wakae pamoja na kukubaliana kuhusu idadi moja ya fonimu na viashiria vyake kulingana na nadharia na kanuni muwafaka. Mabaraza ya Kiswahili yamesisitizwa yasimamiekwa makini sera ya Kiswahili na kuupitia upya usanifishaji wa Kiswahili ili kuweka makubaliano ya pamoja na kuepukana na tatizo la kutofautianakwa idadi ya fonimu na viashiria vyake katikaKiswahili sanifu.

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Khadija Katele
Date Deposited: 13 Sep 2024 11:02
Last Modified: 13 Sep 2024 11:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4197

Actions (login required)

View Item View Item