Zubeir, Salim Khamis
(2023)
Kuchunguza Dhamira za lugha ya Utani katika Masoko ya kuuzia Samaki Kaskazini Pemba.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu imehusu: Kuchunguza dhamira za lugha za utani katika masoko ya kuuzia samaki Kaskazini Pemba. Kwa mnasaba wa mada hii, utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi mawili: (i) Kuchambua dhamira za lugha ya utani katika masoko ya kuuzia samaki Kaskazini Pemba na (ii) Kubainisha mbinu za kisanaa za lugha za utani katika masoko ya kuuzia samaki Kaskazini Pemba. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu za ushuhudiaji, usaili na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kushadadiwa na nadharia za Mwitiko wa Msomaji na Simiotiki. Matokeo ya yanaonesha kwamba, kwa upande wa dhamira zilizojitokeza katika utani wa masoko ya kuuzia samaki kisiwani Pemba ni kujenga umoja na mshikamano, kuelimisha jamii, kuburudisha jamii, ustahamilivu katika kazi, ujasiri, ukombozi, kuoyonya jamii na nyenginezo. Aidha, mbinu za kisanaa zilizobainika ni matumizi ya tashibiha, taswira, takiriri, ishara, kejeli, misemo, methali na tashtiti. Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo ya kufanya utafiti zaidi katika eneo la kipera cha utani ambacho kipo katika utanzu wa sanaa za maonesho ambacho ni muhimu kwa kukuza na kuendeleza utamaduni katika jamii mbali mbali.
Maneno Muhimu: Utani, dhamira, mbinu za kisanaa
Actions (login required)
|
View Item |