Kuchunguza Fani ya Biblia Katika Fasihi Andishi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo.

Msangi, Emmanuel Oscar (2023) Kuchunguza Fani ya Biblia Katika Fasihi Andishi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of PhD EMMANUEL OSCAR MSANGI.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (2MB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa Kuchunguza Fani ya Biblia katika Fasihi Andishi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Tamthiliya Teule za Emmanuel Mbogo. Katika kulifikia lengo kuu la utafiti kulikuwa na malengo mahsusi matatu. Malengo hayo yalikuwa: kubainisha fani za Biblia katika tamthiliya teule za Emmanuel Mbogo, kutafuta sababu za kujitokeza kwa fani za Biblia katika tamthiliya teule za Emmanuel Mbogo pamoja na kubainisha dhamira zinazojidhihirisha kutokana na kuhusishwa kwa fani za Biblia katika tamthiliya teule. Katika utafiti huu ilitumika sampuli moja; sampuli lengwa. Sampuli lengwa ilirejea Biblia na maandiko ya Emmanuel Mbogo yaani Tanzia ya Patrice Lumumba (2015), Wangari Maathai (2015), Mtumwa hadi Siti Binti Saad (2016), Nyota ya Tom Mboya (2016), Malkia Bibi Titi Mohamed (2016) na Mondlane na Samora (2016). Ukusanyaji, uchambuzi na mjadala wa data uliongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu moja, mbinu ya usomaji matini. Mkabala wa kimaelezo ndiyo ulitumika kuchambua data za utafiti huu. Kimsingi, matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna fani nyingi za Biblia katika tamthiliya za Emmanuel Mbogo. Vipengele vya kifani ndivyo vilitumika katika kuchanganua Ubiblia huo: nukuu za Biblia, wahusika wa Biblia, hadithi za Biblia, sajili ya Biblia na mandhari ya Biblia. Tamthiliya zote sita zilizotafitiwa, taswira ya Biblia imeonekana ndani yake. Mathalani simulizi ya kuzaliwa na kufa kwa Yesu Kristo katika Biblia huko Uyahudi zimesikika katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya. Wafuasi wa Nadharia ya Mwingilianomatini wanaeleza kuwa kazi yoyote ya fasihi ni zao la kazi tangulizi (Kristeva, 1981). Kimsingi, tulibaini athari ya kitabu cha Biblia katika tamthiliya teule zilizoandikwa zaidi ya miaka 2000 mbele tangu Biblia iandikwe. Pia utafiti umebaini kwamba, fani za Biblia mbalimbali alizohusisha mtunzi teule katika kazi zake zililenga kuwasilisha dhamira fulani kwa hadhira. Mfano, umuhimu wa kutunza historia katika jamii. Emmanuel Mbogo ameandika tamthiliya nyingine karibuni kama vile tamthiliya ya Julius Nyerere Kizimbani (2022) na Mwinyi na Manyani ya Adili (2022). Tunapendekeza tafiti nyingine zifanyike ili kuendelea kustawisha uga wa fasihi andishi kupitia maandiko ya mwandishi teule.

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Aug 2024 16:51
Last Modified: 29 Aug 2024 16:51
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4058

Actions (login required)

View Item View Item