Kuchunguza Mafanikio na Changamoto za wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili

Awhida, Husin H. H. (2024) Kuchunguza Mafanikio na Changamoto za wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of HUSIN HAMED HUSIN AWHIDA.doc] Microsoft Word - Submitted Version
Download (457kB)

Abstract

Utafiti huu ulichunguza mafanikio na changamoto za wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili na kupendekeza mikakati ya kukuza na kuendeleza Kiswahili katika nchi ya Libya. Malengo mahususi yalikuwa manne ambayo ni kubainisha mafaniko ya wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili, kufafanua changamoto zinazowakabili wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili, kuelezea namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wahitimu wa Kilibya wa shahada za juu za Kiswahili na kupendekeza mikakati ya kukuza na kuendeleza Kiswahili katika nchi ya Libya. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usaili, hojaji na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yamebainisha mafanikio waliyopata wahitimu ni pamoja na kupata kazi ya uhadhiri katika vyuo vikuu nchini Libya, kuandika vitabu na makala za Kiswahili, kuajiriwa katika wizara na balozi, kujiajiri katika ujasiriamali na biashara ndogondogo, kukuza utengamano, kupatikana kwa maprofesa wa Kiswahili wa Kilibya, uongozi katika chuo kikuu na idara na kujenga ushirikiano na vyuo vikuu nya ndani na nje ya nchi. Changamoto wanazokumbana nazo ni kukosekana kwa kamusi ya Kiswahili Kiarabu, tatizo la umilisi wa lugha ya Kiswahili, uhaba wa machapisho ya Kiswahili, kuondoka kwa walimu wazawa wa Kiswahili katika nchi ya Libya, muda wa masomo kuwa mfinyu na ukosefu wa ajira. Utatuzi wa changamoto hizi ni kuandika kamusi ya Kiswahili na Kiarabu kwa kushirikiana na wabobezi wa kamusi, kupata muktadha mpana wa matumizi ya Kiswahili ili kukuza umilisi, kuandika machapisho ya Kiswahili yenye muktadha wa Kilibya, kuwarudisha walimu wazawa wa Kiswahili katika nchi ya Libya, kuongeza muda wa masomo na kujiajiri ili kukabiliana na ukosefu wa ajira rasmi. Mikakati ya kukuza na kuendeleza Kiswahili ambayo imependekezwa ni pamoja na kuanzisha chombo cha kusimamia Kiswahili, kuanzisha idhaa ya Kiswahili katika shirika la utangazaji la Libya, kurudisha somo la Kiswahili katika elimu ya sekondari, kuanzisha chama cha wanataaluma wa Kiswahili, kuandaa matamasha ya sanaa na utamaduni, kufunguwa ubalozi wa Tanzania nchini Libya na kuunda sera ya lugha ya Kiswahili nchini Libya.

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Khadija Katele
Date Deposited: 12 Aug 2024 11:00
Last Modified: 12 Aug 2024 11:00
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3940

Actions (login required)

View Item View Item