Sekemi, Paulina
(2023)
kuchunguza ukiushi wa tafsiri katika mabango kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili katika mkoa wa Arusha.
UNSPECIFIED thesis, UNSPECIFIED.
|
PDF
- Submitted Version
Restricted to Registered users only
Download (3MB)
|
Abstract
Taaluma ya tafsiri inakuwa siku hadi siku, hali inayofanya wataalamu mbalimbali kushughulikia tafsiri katika maeneo tofauti kama vile fasihi na isimu kulingana na uhitaji na uzito wa taaluma hii. Utafiti huu umechunguza “Ukiushi wa Tafsiri katika Mabango kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwa wakazi wa mkoa wa Arusha. Aidha, utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Arusha, wilaya ya Arusha mjini, kata ya Mjini kati na Ngarenaro. Nadharia ya Usawe na Athari Sawa ndiyo iliyotuongoza katika uchambuzi wa data. Data zilizotumika katika utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia ya ushuhudiaji. Vilevile, mahojiano yaliweza kutumika ili kuwezesha kupata data toshelevu kutoka kwa watoa taarifa. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa
kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa upo ukiushi wa aina mbalimbali katika mabango yaliyoandikwa Kiingereza na kutafsiriwa Kiswahili. Ukiushi uliojitokeza ni pamoja na ukiushi wa kisemantiki ambao ulijitokeza kwa kiasi kikubwa ikifuatiwa na ukiushi wa kimofolojia, ukiushi wa kufanya tafsiri sisisi na ukiushi wa kisintaksia.Kutokana na matokeo ya utafiti huu inapendekezwa kuwa utafiti mwingine unaweza kufanywa katika mikoa mingine hususani jiji la Dar es Salaam ambako ni kitovu cha biasharanchiniTanzania ili kuweza kudhihirisha endapo kuna ukiushi wa tafsiri katika mabango kama zilizobainika katika utafiti huu au l
Actions (login required)
|
View Item |