Enocy, Edward L.
(2022)
Kutathimini Uhusiano wa Kifonetiki Baina ya Kisukuma cha Ng’weli na Kisukuma cha Ntuzu.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulilenga kutathimini uhusiano wa kifonetiki baina ya Kisukuma cha Ng’weli na Kisukuma cha Ntuzu kwa kuchunguza na kuchambua sauti zenye kuchukuliana nafasi miongoni mwa maneno ya lahaja hizi mbili. Malengo yalikuwa kuchunguza ni kwa namna gani hufanana kifonetiki na namna hutofautiana kisha kupima kiwango cha kuachana na kutofautiana kifonetiki. Utafiti huu ulifanyika katika kijiji cha Nkololo kilichopo wilayani Bariadi na kijiji cha Nyamalimbe kilichopo katika wilaya ya Geita vijijini. Katika kufikia adhima hii, data zilikusanywa kutoka kwa watafitiwa kwa njia ya hojaji, usaili, udodosaji pamoja na uchunguzi. Nadharia mbili zimetumika katika utafiti; fonolojia zalishi na Makutano na Mwachano yenye kutumika kulinganisha lugha au lahaja zenye asili moja. Nadharia ya Makutano na mwachano inaeleza jinsi lugha za Ki-Bantu zilivyoachana kutoka katika chimbuko lake, zikatawanyika na hatimaye kuwa lugha tofauti, lakini kadri zilivyoendelea kusambaa baadhi yake zikakutana tena na kuonekana kama lahaja za lugha moja. Utafiti huu umebaini kuwa kuna mfanano mkubwa wa kifonetiki baina ya Kisukuma cha Ntuzu na Kisukuma cha Ng’weli. Hii ni kwa sababu sauti zenye kuchukuliana nafasi katika msamiati wa Kisukuma cha Ntuzu na Kisukuma cha Ng’weli huwa na sifa nyingi bainifu za kifonetiki zenye kufanana kuliko kiwango cha sifa hizo kutofautiana. Hii inathibitisha kwamba, maneno ya lahaja hizi mbili huwa aghalau na sauti moja au zaidi zinazotofautiana miongoni mwake lakini sauti hizi huwa na sifa nyingi za kifonetiki zenye kufanana. Mtafiti alipendekeza kuwa kunahitajika kufanyika utafiti wa mifanyiko ya kifonolojia katika lugha ya Kisukuma pamoja na lahaja zake.
Manene muhimu: Uhusiano, Ng’weli, Kisukuma, Ntuzu.
Actions (login required)
|
View Item |