Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Jamii ya Kiuyu Maambani.

Mohamed, Zuhura Saidi (2022) Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Jamii ya Kiuyu Maambani. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA ZUHURA SAID.pdf] PDF - Submitted Version
Download (586kB)

Abstract

Utafiti huu umechunguza Dhima za Nyimbo za Nyiso za Jamii ya Kiuyu Maambani. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni:- Kubainisha nyiso zinazoimbwa katika jamii ya Kiuyu Maambani, Kueleza dhamira zinazojitokeza katika nyiso za jamii ya Kiuyu Maambani na Kufafanua dhima za nyiso zinazoimbwa katika jamii ya Kiuyu Maambani. Utafiti huu ulikuwa ni wa uwandani ambapo data zake zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili. Mtafiti alifanya usaili na wanawake 20 wa Kiuyu Maambani ambao wamewahi kuhudhuria mafunzo ya unyago ambayo yanaambatana na nyiso. Jumla ya nyimbo 30 zilikusanywa na baadae mtafiti aliteua nyimbo 17 ili kutumika kuwa sampuli ya utafiti huu. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Vile vile, utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwitiko wa Msoamaji. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kwa kutumia kigezo cha dhima, nyimbo za nyiso za jamii ya Kiuyu Maambani zinaweza kuwekwa katika makundi ya nyimbo zinazofunza usafi, nyimbo zinazokuza umoja na mshikamano, nyimbo zenye kuonya, nyimbo zenye kuhamasisha kazi, nyimbo zinazofunza maisha ya ndoa na nyimbo zinazoendeleza utamaduni wa jamii. Dhamira zinazopatikana katika nyimbo za nyiso za jamii ya Kiuyu Maambani ni za utamaduni, mapenzi na ndoa, usafi, uaminifu katika ndoa, kuondoa woga, umoja na mshikamano na dhamira ya kazi.” Matokeo ya utafiti huu yameonesha pia kuwa nyimbo za nyiso za jamii ya Kiuyu Maambani zina dhima za kukuza mshikamano katika jamii, kuhimiza ustahamilivu, kubainisha utamaduni wa jamii, kuhimiza ujasiri amali, kufundisha maadili mema na kuburudisha. Mwisho, utafiti unahitimisha kwamba nyimbo za ngoma ya nyiso za jamii ya Kiuyu Maambani ni muhimu sana katika kuwafanya wanawake kuwa na maadili bora ya maisha yao ya ndoa na jamii kwa ujumla. Maneno Makuu: Nyiso, Nyimbo, Dhima

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 10:11
Last Modified: 05 May 2023 10:11
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3624

Actions (login required)

View Item View Item