Kuchunguza Fani na Dhamira katika Ushairi wa Kiswahili: Mifano kutoka Diwani za Dhifa na Wasakatonge.

Alhabib, Emhemad Abdallah (2022) Kuchunguza Fani na Dhamira katika Ushairi wa Kiswahili: Mifano kutoka Diwani za Dhifa na Wasakatonge. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of EMHEMAD ABDALLAH AHABIB MPYA KABISA.pdf] PDF - Submitted Version
Download (593kB)

Abstract

Mada ya utafiti huu ulihusu kuchunguza fani na dhamira katika ushairi wa Kiswahili kwa kurejelea diwani za Dhifa ilyoandikwa na Euphrase Kezilahabi na Wasakatonge ya Mohamed Khatib. Utafiti wetu ulikuwa na malengo mahsusi matatu yaliyolenga; kubainisha kufanana kwa matumizi ya fani katika mashairi ya Dhifa na Wasakatonge, kuelezea kutofautiana kwa matumizi ya fani katika mashairi ya dhifa na Wasakatonge; nakulinganua dhamira katika mashairi ya Dhifa na Wasakatonge. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Uchambuzi na uhakiki wa data zilizowasilishwa ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia za Simiotiki na Usosholojia. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa watunzi wote wawili wana matumizi ya mtindo, muundo, wahusika, lugha na mandhari. Aidha, wamefanana na kutofautiana katika matumizi ya vipengele hivyo kwa kiasi fulani. Dhamira zilizojitokeza katika diwani zote ni uongozi, ukabila na udini, rushwa, maisha na nafasi ya mwanamke. Pia, watunzi wanafanana na kutofautiana si kwa kiasi kikubwa katika baadhi ya dhamira. Tasinifu hii inapendekeza kuwa utafiti kama huu ufanywe kwa kulinganisha na kulinganua fani na dhamira katika diwani nyingine za watunzi hawa wawili. Pia, unaweza kufanywa katika diwani za washairi wengine wa ushairi wa Kiswahili na wa ushairi wa kigeni. Maneno Muhimu: Fani, Dhamira, Diwani

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 10:03
Last Modified: 05 May 2023 10:03
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3623

Actions (login required)

View Item View Item