Muundo wa Kirai Kitenzi katika Lugha ya Kindali.

Kibona, Denis (2022) Muundo wa Kirai Kitenzi katika Lugha ya Kindali. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of DENIS KIBONA.pdf] PDF - Submitted Version
Download (498kB)

Abstract

Utafiti huu unahusiana na muundo wa kirai kitenzi cha lugha ya Kindali ambao umefanyika katika wilaya ya Ileje ambapo ndio eneo halisi la wazungumzaji wa lugha hiyo. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya Kindali. Malengo mahususi ni kubainisha vipashio vya muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya Kindali, kuelezea mpangilio wa vipashio vya muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya Kindali, na kujadili dhima za kisarufi za kirai kitenzi cha lugha ya Kindali. Utafiti huu umehusisha wazee kuanzia miaka hamsini (50) na sabini (70), ambao ni wakazi wa kata ya Kafule. Data za utafiti huu zilipatikana kutokana na hojaji zilizotayarishwa ambazo zilikuwa na maswali tofauti yaliyokuwa yanahusiana na kirai kitenzi cha lugha ya Kindali. Watoa taarifa hao walitakiwa kujibu maswali yote ili data sahihi ziweze kupatikana. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa muundo wa kirai kitenzi cha lugha ya Kindali unavipashio vinavyoandamana navyo, vipashio hivyo ni kama vile nomino, kitenzi kisaidizi, kitenzi kikuu, kivumishi, kielezi na sentensi. Utafiti huu umependekeza kuwa ufanyike utafiti ambao unahusu kirai kihusishi cha lugha ya Kindali kwa kutumia nadharia ya x- baa. Maneno Makuu: Kitenzi, Kirai, Sentensi

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 09:57
Last Modified: 05 May 2023 09:57
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3622

Actions (login required)

View Item View Item