Tathmini Linganifu ya Umilisi wa Kiisimu wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Uchunguzi kifani kutoka Mufindi.

Tagalile, Alex (2022) Tathmini Linganifu ya Umilisi wa Kiisimu wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Uchunguzi kifani kutoka Mufindi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ALEX  TAGALILE.pdf] PDF - Submitted Version
Download (887kB)

Abstract

Utafiti huu ulilenga kufanya tathmini linganifu ya umilisi wa isimu ya Kiswahili kama lugha ya pili kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya umilisi wa mawasiliano ya Canale na Swain (1980, 1981), ili kuweza kutimiza malengo ya utafiti huu na pia kujibu maswali ya utafiti huu. Data zilikusanywa kwa njia ya jaribio la umilisi na dodoso. Eneo la utafiti lilikuwa wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwenye shule za sekondari tano za serikali. Watafitiwa walikuwa ni wanafunzi kidato cha tatu 115, wasichana 60 na wavulana 55 walioteuliwa kinasibu. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kitakwimu. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa wanafunzi wa kike wana ujuzi na ubobezi juu zaidi ya wale wa kiume katika nyanja nyingi sana za kiisimu zilizopimwa. Hali kadhalika utamalaki huu wa wanafunzi wa kike umeonekana katika vichocheo viliyoonekana kusababisha ufanisi wa umilisi isimu isipokuwa ukaririshaji wa yaliyofundishwa darasani, ambayo ni kikwamizo cha umilisi katika lugha, na ambamo wavulana ndio waliotamalaki kiidadi. Hata hivyo, makundi yote mawili yalifanana katika kukataa kwamba utoshelevu wa vitabu darasani ni kichocheo cha umilisi isimu ya Kiswahili kwao. Utafiti ulifikia hitimisho kuwa kuna utofauti mkubwa wa kijinsia katika umilisi wa lugha kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili na kuwa jinsia ya kike ndiyo yenye fanaka zaidi. Tumependekeza uboreshaji wa pedagojia ya Kiswahili na tafiti linganishi zifanyike pia kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni na pia kuhusu umilisi katika wigo wa Kiswahili cha mazungumzo. Maneno Makuu: Umilisi, Isimu, Kijinsia

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 09:44
Last Modified: 05 May 2023 09:44
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3620

Actions (login required)

View Item View Item