Athari za Kimofofonolojia za Lugha ya Kirundi Katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Jamiilugha ya Kirundi.

Bizimana, Jean (2022) Athari za Kimofofonolojia za Lugha ya Kirundi Katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Jamiilugha ya Kirundi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Jean Bizimana.pdf] PDF - Submitted Version
Download (708kB)

Abstract

Utafiti huu ulitathmini Athari za Kimofofonolojia za Lugha ya Kirundi Katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Jamii lugha ya Kirundi katika baadhi ya vyuo vikuu. Malengo mahususi katika utafiti huu ni (1) Kubainisha athari za kimofofonolojia ya Kirundikatika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 kwa wanafunzi wa jamiilugha ya Kirundi; (2) Kutathmini viwango vya utamalaki wa aina mbalimbali za athari za Kimofofonolojia za Kirundi katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 kwa wanafunzi wa jamiilugha ya Kirundi., na (3) kubainisha juhudi za walimu kubaini na kukabiliana na aina hizi za athari. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Linganishi. Ili kufikia malengo yake, wanafunzi mia moja wa vyuo vikuu vitatu walihusishwa pamoja na wahadhiriwa Kiswahili wanane. Michakato ya usampulishaji iliyotumiwa ni usampulishaji usio nasibu na usampulishaji nasibu. Mbinu za kukusanyia data zilikuwa hojaji, jaribio la umilisi na ushuhudiaji. Uchanganuzi wa data ulionyesha kuwa athari za kimofofonolojia zinazoibuka katika kazi za Kiswahili za wanafunzi wa jamiilugha ya Kirundi wanaojifunza Kiswahili yalihusu uchopekaji, udondoshaji na matumizi ya fonimu mbadala. Aghalabu athari za kimofofonolojia zilizodhihirika zilisababishwa na uhawilishaji wa L1 ya mwanafunzi kwa kuhamisha baadhi ya kanuni za kiisimu za L1 hadi L2. Katika kuangazia mbinu za kutumiwa na walimu ili kuwasaidia wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama L2, walimu watafititiwa walibaini mbinu za hatua kwa hatua; yaani stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Maneno Makuu: Kimofofonolojia, Fonimu, Uchopekaji

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 09:39
Last Modified: 05 May 2023 09:39
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3619

Actions (login required)

View Item View Item