Kuchunguza Dhima za Utani wa Jadi Kati ya Watu wa Kiuyu Minungwini na Kojani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Juma, Bimize Hamad (2022) Kuchunguza Dhima za Utani wa Jadi Kati ya Watu wa Kiuyu Minungwini na Kojani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of BIMIZE HAMAD JUMA.pdf] PDF - Submitted Version
Download (576kB)

Abstract

Tasnifu hii inahusu Kuchunguza Dhima za Utani wa Jadi Kati ya Watu wa Kiuyu Minungwini na Kojani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Simiotiki na ndharia ya Mwitiko wa Msomaji. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na usomaji makini. Hivyo, matokeo yalikuwa kama ifuatavyo. Lengo mahsusi la kwanza la Utafiti huu lilikuwa ni: Kubainisha aina za utani wa jadi katika jamii ya Kiuyu Minungwini na Kojani. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa utani wa jadi wa jamii ya Kiuyu Minungwini na Kojani unaweza kuwekwa katika utani wa misibani, utani wa shuguli za harusi, utani kwenye minada ya bidhaa, utani katika shughuli za uvuvi, utani unaohusu kujitambulisha, utani katika michezo, utani katika kuchumbia wachumba, utani wa matukio ya ajali na huzuni, utani katika vyombo vya usafiri na utani katika shughuli za kilimo. Lengo mahsusi la pili la utafiti huu lilikuwa ni: “Kuchunguza vipengele vya lugha vinavyojitokeza katika utani wa jadi kati ya wanajamii wa Kiuyu Minungwini na Kojani.” Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa utani wa jadi katika jamii ya Kiuyu Minungwini na Kojani unatumia vipengele vya lugha ambavyo ni lugha ya lahaja, lugha ya kishairi, balagha, dhihaka na lugha ya matusi. Lengo mahsusi la tatu la utafiti huu lilikuwa ni: “Kuchambua dhima za utani wa jadi kwa jamii ya watu wa Kiuyu Minungwini na Kojani.” Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa utani wa jadi wa jamii ya Kiuyu Minungwini na Kojani una dhima kukuza lugha ya Kiswahili, kuendeleza utamaduni, kukuza fasihi ya Kiswahili, kutambulisha na kuifunza jamii. Dhima nyengine ni pamoja na kukuza umoja na mshikamano, kuhimiza kazi na kuweka hakiba, kuikosoa jamii, kuendeleza mila na desturi za jamii na kuburudisha. Mwisho, utafiti umependekeza kufanyika kwa tafiti zaidi kuhusu fani ya utani na jamii kutumia lugha isiyokuwa na matusi ili kuleta athari chanya ya utani. Maneno Makuu: Utani, Desturi, Simiotiki

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 06:42
Last Modified: 05 May 2023 06:42
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3602

Actions (login required)

View Item View Item