Kuchunguza Dhamira na Matumizi ya Lugha katika Nyimbo za Ngoma ya Msewewa Kambini Kichokochwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Hamad, Hamad Bakari (2022) Kuchunguza Dhamira na Matumizi ya Lugha katika Nyimbo za Ngoma ya Msewewa Kambini Kichokochwe Mkoa wa Kaskazini Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of HAMAD BAKAR HAMAD.pdf] PDF - Submitted Version
Download (611kB)

Abstract

Utafiti huu ulijikita Kuchunguza Dhamira na Matumizi ya Lugha katika Nyimbo za Ngoma ya Msewe wa Kambini Kichokochwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba.Ili kukamilika kwa utafiti huu, mtafiti alikuwa na madhumuni mahususi matatu ambayo ni kubainisha nyimbo za ngoma ya Msewe wa Kambini Kichokochwe, Kubainisha dhamira katika nyimbo za Ngoma ya Msewe wa Kambini Kichokochwe na kufafanua vipengele vya lugha katika nyimbo za mse wa Kambini Kichokochwe. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia njia ya usaili na njia ya usomaji makini. Data hizo zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Vile vile, njia za kimaktaba zilitumika kwa mtafiti kwa ajili ya kujisomea kazi tangulizi na maandiko tofauti kwa lengo la kujiongezea maarifa na kufanikisha utafiti wake. Nadharia zilizotumika ni Simiotiki na Mwitiko wa Msomaji. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa kwa kutumia kigezo cha dhima, nyimbo za ngoma ya msewe wa Kambini Kichokochwe Mkoa wa Kaskazini Pemba zinaweza kuwekwa katika makundi ya nyimbo za siasa, nyimbo zinazokuza umoja na mshikamano, nyimbo za kusifia, kukejeli, nyimbo zinazokuza utamaduni, nyimbo zinazofichua maovu, nyimbo za maadili na nyimbo zinazoonya jamii. Kwa upande wavipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo hizo, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa nyimbo za ngoma ya Msewe wa Kambini Kichokochwe Mkoa wa Kaskazini Pemba zinatumia vipengele vya lugha ya lahaja, matumizi ya taswira, lugha ya balagha, kejeli, tashihisi na takiriri. Vile vile, utafiti umebaini kuwa nyimbo za ngoma ya Msewe wa Kambini Kichokochwe zina dhamira za kusifu, maadili, umoja na mshikamano, kuifunza jamii, siasa, kazi, ngono holela nakuonya. Mwisho, utafiti unapendekeza kwamba ipo nafasi ya kufanya tafiti nyengine katika nyimbo hizo. Maneno Makuu: Ngoma, Simiotiki, lahaja

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 06:35
Last Modified: 05 May 2023 06:35
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3601

Actions (login required)

View Item View Item