Malezi Ya Watoto Enzi Za Wazanzibari Wa Kale.

Taher, Mohammed Amhammed Mohammed Ali (2021) Malezi Ya Watoto Enzi Za Wazanzibari Wa Kale. Sebha University Journal of Human Sciences, VOL.20 (NO. 2).

[thumbnail of 2021-19-02-013MALEZI  YA  WATOTO  ENZI  ZA   WAZANZIBARI   WA   KALE فى السواحلية مجلة سبها 2022.pdf] PDF - Submitted Version
Download (675kB)

Abstract

Maandalizi ya malezi ya watoto enzi za wazanzibar wa kale yalianza mapema mara mwanamke anapochukuwa uja uzito. Mjamzito aliandaliwa mambo maalumu kama chakula chake , nguo ,sehemu maalumu ya kukaa ili ajifungue salama na kuanza kumlea mwana. Naye mwana aliyezaliwa alikuta ameshaandaliwa mambo yanayomhusu na hupokelewa kwa dua na shangwe toka kwa wanafamilia na wengine. Alipelekwa madrasa kujifunza kusoma kurani tukufu na elimu nyingine za maadili ya kiislamu ambazo ndizo zilizokuwa msingi mkuu wa kurekebisha maadili yake. Pamoja na haya alifundishwa kivitendo kuheshimu wengine katika jamii kwa kadri ya hadhi zao . Alipelekwa shule kujifunza elimu za mazingira na sayansi mbali mbali pamoja na lugha za kigeni na sanaa mchanganyiko ili kumjenga kimaarifa na kumwandaa kuitumikia jamii. Watoto walipobaleghe walipelekwa jandoni, kwa watoto wa kiume, na unyagoni kwa watoto wa kike. Huko walifunzwa namna ya kukabiliana na mabadiliko yaliyojitokeza katika miili yao na namna ya kuishi katika jamii wakiwa watu wazima tayari kuanzisha familia pindi muda utakapowadia. Malengo makuu ya malezi haya yalikuwa kumtayarisha mtoto kuishi maisha ya maadili mema katika jamii na kutoa mchango wake kwa kadiri ya nafasi yake katika jamii husika

Item Type: Article
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 May 2023 06:29
Last Modified: 05 May 2023 06:29
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3600

Actions (login required)

View Item View Item