Bakari, Mtoro Mchukivu
(2022)
Changamoto za Utohoaji wa Maneno ya Kiingereza Katika Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii ilikuwa na lengo kuu la kuchunguza changamoto za utohoaji wa maneno ya Lugha ya Kiingereza katika lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Katika kufikia lengo kuu hilo, malengo mahususi matatu yamehusishwa ambayo ni kubainisha mbinu za utohoaji wa maneno ya Kiingereza katika lugha ya Kiswahili, pili, kuelezea athari za utohoaji wa maneno ya Kiingereza katika lugha ya Kiswahili na tatu, kufafanua changamoto za utohoaji wa lugha ya Kiingereza kwenye lugha ya Kiswahili. Utafiti huu ulifanyika katika taasisi za umma zinazojihusisha na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania ambazo ni BAKITA na TATAKI ambazo zote zipo mkoani Dar es Salaam. Njia zilizotumika kuwapata watoa taarifa ni usampulishaji nasibu na usi nasibu. Usampulishaji nasibu ulitumika kwa wasimamizi wakuu wa idara. Usampulishaji usio nasibu ulitumika kwa wafanyakazi wa idara. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mkabala wa Mlingano Chanzi ulioasisiwa na Smith, mwaka 2006. Nadharia hii imechaguliwa na mtafiti kwani ina uwezo unaoruhusu mikakati mbalimbali urekebishaji wa maneno yaliyotoholewa. Katika ukusanyaji wa data kutoka katika eneo la utafiti, mtafiti alitumia njia ya mahojiano na dodoso. Jumla ya watafitiwa waliohusika katika utafiti huu walikuwa ni 43. Utafiti huu umebaini kuwa utohoaji wa maneno hutokana na kuibuka kwa dhana mpya katika jamii za kilimwengu kutokana na ukuaji wa kimaendeleo.
Maneno Makuu: Kutohoa, mlingano chanzi, Kiswahili, Kiingereza
Actions (login required)
|
View Item |